Monday, November 26, 2012

"BREAKING NEWS" SHARO MILIONE AFARIKI DUNIA KTK AJALI






 Msanii  Sharo MIlionea enzi  za uhai  wake
 Msanii  Sharo Milionea (kulia) akiwa na pacha  wake mzee  King Majuto
 BAADA  ya  kifo cha msanii  Stivin Kanumba  tasnia ya Filam ama  kundi la Bongo Movie  limepata  pigo jingine  kubwa  baada ya msanii wa maarufu nchini  kupitia  kundi la Bongo Movie Sharo Milionea  kupoteza maisha katika ajali mbaya ya gari  iliyotokea usiku  wa  jumatatu mkoa  wa Tanga.


Sharo Milionea  amepata ajali  hiyo  katika  kijiji cha .Lusanga, Muheza  mkoani Tanga kifo ambacho  kimewagusa  watanzania  waliowengi kutokana na umaarufu  wa ghafla ambao msanii  huyo alitokea  kuupata  akiwa na pacha  wake  wa karibu mzee  King Majuto .

Katika mkoa  wa Iringa  wadau  na  wasomaji  wa mtandao  huu  wa www.francisgodwin.blogspot.com  wameeleza  kusitushwa na taarifa  hiyo ya  kifo cha msanii  huyo  huku baadhi yao  wakishindwa  kuamini taarifa  hizo  za  kicho  cha msanii  huyo.

Huku  watangazaji wa  radio  mbali mbali mkoani Iringa na nchi ya mkoa  wa Iringa  wakionyesha  kushindwa kumudu  kuendelea na vipindi  vyao  kutokana na  majonzi waliyokuwa nayo  juu ya  kifo cha msanii  huyo.
Msanii aliyekuja juu kwa kasi kwa muziki na pia matangazo ya biashara likiwemo la Airtel Money la kampuni ya simu ya Airtel aliyejulikana kwa jina la Sharobaro a.k.a Sharo Milionea
Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Afande Constatine Masawe, amethibitisha  kutokea kwa  kifo cha  wa Sharobaro, kufuatia  ajali ya gari  katika kijiji cha Lusanga, Muheza, mkoani Tanga  ambako ndio nyumbani
"Kifo cha millionea kimetokea majira ya saa mbili, eneo linaloitwa Maguzoni songa , akiwa anaendesha gari aina ya  toyota Harrier akitokea Dar  kuelekea Muheza, alipofika hapo gari liliacha barabara na kupinduka, na maiti imehifadhiwa katikachumba cha maitiya  Hospitali teule ya Muheza.... alikuwa mwenyewe."BOFYA HAPA

Sunday, November 25, 2012

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU
TAARIFA YA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961 - 2011)
MKOA WA IRINGA
NOVEMBA, 2011
Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa
VIONGOZI WA SASA WA MKOA WA IRINGA
MKUU WA MKOA
MHE. DR. CHRISTINE
G. ISHENGOMA (MB)
KATIBU TAWALA WA
MKOA
BIBI. GERTRUDE K.
MPAKA
MAKATIBU TAWALA WASAIDIZI WA MKOA
Sehemu ya Sehemu ya Mipango
Rasilimali Watu na Uratibu
Bw. Barnabas Bw. Nuhu
Ndunguru Mwasumilwe
Sehemu ya
Miundombinu
Sehemu ya Sehemu ya Sehemu ya Uchumi
Huduma za Jamii Serikali za Mitaa na Uzalishaji
Dr. Ezekiel Bibi. Wamoja Bw. Adam Swai
Mpuya Ayubu
Bw. Vicent.
James
WAKUU WA WILAYA
Mkuu wa Wilaya ya
Iringa
Mhe. Capt Aseri
Msangi
Mkuu wa Wilaya Mkuu wa Wilaya Mkuu wa Wilaya Mkuu wa wilaya ya
ya Njombe ya Makete ya Ludewa Mufindi
Mhe. Sarah Mhe.Zainabu Mhe. Georgina Mhe. Evarista
Dumba Kukwega Bundala Kalalu
ii
YALIYOMO
VIFUPISHO ............................................................................................................ v
SHUKRANI ............................................................................................................ vi
DIBAJI .................................................................................................................. vii
SURA YA 1 ........................................................................................................... 1
1.0
HISTORIA FUPI YA MKOA: ................................................................. 1
1.1
Mahali Mkoa ulipo.............................................................................. 1
1.2. Eneo la Mkoa ........................................................................................... 1
1.3. Utawala ..................................................................................................... 2
1.4. Idadi ya watu .......................................................................................... 2
1.5 Hali ya hewa ............................................................................................. 4
1.6
Udongo ................................................................................................. 5
1.7.
Shughuli za Kiuchumi ...................................................................... 6
1.8.
Pato la Mkoa wa Iringa .................................................................... 6
SURA YA 2. ......................................................................................................... 8
2.0: MUUNDO WA MKOA ULIVYOBADILIKA KATIKA NYAKATI
TOFAUTI KUANZIA 1961 ................................................................................. 8
2.1 Madaraka Mikoani:.................................................................................. 8
2.2 Vijiji na Madaraka Vijijini: .................................................................... 9
2.3: Sekretarieti za Mikoa: ........................................................................ 10
2.4: Hali ya Uongozi na Utawala kuanzia 1961;................................. 10
2.5: Viongozi wa sasa wa mkoa wa Iringa ........................................ 13
SURA YA 3. ....................................................................................................... 14
3.0:
MAJUKUMU NA MALENGO YA MKOA ............................................. 14
3.1:
Dira ya Mkoa.................................................................................... 14
3.2: Dhamira ya Mkoa ............................................................................ 14
3.3: Majukumu ya Mkoa ........................................................................ 14
3.4: Mikakati ya Mkoa............................................................................. 15
SURAYA 4.......................................................................................................... 17
4.0:
MABADILIKO NA MATUKIO MAKUU KATIKA MFUMO WA
KISIASA, KIULINZI, KIUTAWALA, KIUCHUMI, KITEKNOLOJIA NA
KIJAMII................................................................................................................. 17
4.1: Mafanikio yaliyopatikana hadi sasa ........................................... 17
4.2 Utawala Bora ......................................................................................... 19
4.3 Utekelezaji wa Mipango na Bajeti .................................................... 21
4.4. Huduma za kiuchumi .......................................................................... 21
4.5. Huduma za Jamii .................................................................................. 35
4.5.2 Afya ........................................................................................................ 38
4.6. Miundombinu na Barabara ................................................................ 42
4.7. Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ............................................ 44
5.0 MAKUNDI MAALUM YALIYOSHUGHULIKIWA KATI YA 1961
2010 ...................................................................................................................... 45
5.1 Watoto ...................................................................................................... 45
5.2 Wazee ....................................................................................................... 45
5.3 Walemavu ................................................................................................ 46
iii
SURAYA 6.......................................................................................................... 47
6.0. HALI YA UKIMWI ...................................................................................... 47
6.1 Muelekeo wa mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya VVU
na janga la UKIMWI Mkoani: .................................................................... 47
6.2 Kazi zilizotekelezwa katika kipindi cha mwaka 2009/2010:- 48
6.3 Mafanikio yaliyopatikana: ................................................................... 51
6.4 Changamoto: .......................................................................................... 52
6.5 Matarajio .................................................................................................. 53
SURA YA 7. ....................................................................................................... 55
7.0
MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA .................................................. 55
SURA YA 8. ......................................................................................................... 56
8.0
CHANGAMOTO MBALIMBALI:.......................................................... 56
SURA YA 9. ....................................................................................................... 57
9.0: MATARAJIO YA MKOA KATIKA MIAKA 50 IJAYO: .......................... 57
iv
VIFUPISHO
MMEM
MES
ASDP
DADP
MTEF
MKUKUTA
NBS
O & OD
WARC
EPZ
MEMKWA
MMAM
VVU
PMTCT
RCH
FHI
CMAC
WMAC
CTC
MSD
ICT
Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi
Mpango wa maendeleo ya Elimu ya Sekondari
Agriculture Sector Development Program me
District Agriculture Development Plan
Medium Term Expenditure Framework.
Mkakati wa kukuza Uchumi na kupunguza
Umaskini
National Bureau of Statistics
Opportunities and Obstacles to Development
Ward Agriculture Resource Centers
Export Processing Zone
Mpango wa Elimu ya Msingi kwa waliokosa
Mpango wa Maendeleo ya Huduma za Afya ya
Msingi
Virus vya Ukimwi
Prevention of Mother to Child Transmission
Reproductive and Child Health
Family Health International
Council Multi Sectoral HIV/AIDS
Ward Multi - Sectoral HIV/AIDS Committee
Care and Treatment Clinic
Medical store Department
Information and Communication
Technology.
v
SHUKRANI
Kitabu hiki kimeandaliwa na Ofisi ya
Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa kuzingatia
Mwongozo
wa
uandaaji
mafanikio ya miaka
uliotolewa na Ofisi
taarifa
50
ya
ya
ya
Uhuru
Waziri
Mkuu
mwezi Juni mwaka 2011.
Yaliyomo katika kitabu hiki yametokana
na taarifa za mafanikio ya Mkoa katika
kipindi
cha
miaka
50
tangu
tupate
Uhuru. Kazi ya kuandika kitabu hiki hasa ukusanyaji wa takwimu
mbalimbali ilikuwa ngumu lakini yenye mafanikio. Nawashukuru
sana wataalamu wa Ofisi yangu na wadau wengine wote walioshiriki
kwa namna moja au nyingine kutusaidia kupata taarifa zilizohitajika
kwa ajili ya kuandika kitabu hiki. Hasa Bibi Gertrude K. Mpaka
Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa ambaye amesimamia na
kuhakikisha kuwa tunapata takwimu zilizohitajika kwa ajili ya
kuandika kitabu hiki. Amekuwa kiongozi wa mfano.
Nachukua fursa hii pia kushukuru Ofisi ya Waziri Mkuu kwa
Mwongozo
waliotoa
wa
Uandaaji
wa
kitabu
hiki.
Vile
vile
ninawashukuru, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri
za Mkoa wa Iringa kwa kushirikiana nasi kikamilifu katika kuandika
historia ya Mkoa wetu.
Mwisho, napenda kuwaomba wananchi wote wa Mkoa wa Iringa wasome
kitabu hiki ili kujua wapi tumetoka, wapi tulipo na wapi tunakwenda.
TUMETHUBUTU TUMEWEZA NA TUNAZIDI KUSONGA MBELE
Mhe. Dr. Christine Gabriel Ishengoma (Mb.)
Mkuu wa Mkoa wa Iringa
Tarehe 01 Novemba, 2011
vi
DIBAJI
Kitabu hiki kinaelezea hali ya maendeleo
ya Mkoa wa Iringa tangu
Mwaka 1961 hadi Mwaka 2011. Katika
kuwezesha
Mkoa
yaliyowekwa,
kufikia
Mkoa
mbalimbali za
Maendeleo, Ilani
malengo
ulizingatia
Kisekta,
ya
Sera
Mipango
Chama
ya
Tawala,
Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza
Umasikini (MKUKUTA), Dira ya Taifa ya
Miaka 2025 na Mpango Mkakati wa Mkoa na Halmashauri zake zote.
Aidha, maandalizi ya kitabu hiki yamefanyika kwa njia shirikishi kwa
kuwashirikisha wadau wa maendeleo kuanzia ngazi ya Kijiji, Kata,
Tarafa, Wilaya, Mkoa na Taifa. Hatua hii imewezesha upatikanaji wa
taarifa mbali mbali ambazo zimewezesha Mkoa kuandaa taarifa
kamili ya mafanikio kuanzia Mwaka 1961
2011.
Katika kipindi cha kuanzia Mwaka 1961 hadi Mwaka 2011 Mkoa
umekuwa na mafanikio ambayo yamewezesha kuongezeka kwa
pato la Mkoa kutoka Tshs. 5,698,000.00 Mwaka 1961 hadi Tshs.
1,702,430,000.00 Mwaka 2010.
Licha ya Mafanikio haya Mkoa unakabiliwa na changamoto nyingi
kama; kuchelewa kupata fedha za matumizi ya kawaida na miradi
ya
Maendeleo,
kupanda
kwa
bei
za
pembejeo
za
kilimo,
kutopatikana dawa muhimu katika kitengo cha MSD wakati wote,
upungufu wa miundombinu katika shule za msingi na sekondari na
mengineyo.
Tunafanya
jitihada
ya
kukabiliana
na
changamoto
hizi
kwa
kuwasiliana na Wizara ya Fedha ili fedha ziletwe mapema, kuweka
mpango mzuri
na matumizi
kwa fedha kidogo iliyopatikana,
kuwapatia wataalamu mafunzo mbalimbali, na Mipango shirikishi
imekuwa ikiandaliwa kwa kuzingatia vipaumbele.
vii
Ninayo furaha kusema kwamba Mkoa kwa kushirikiana na wadau
mbalimbali unazifanyia kazi changamoto hizi. Ninatarajia katika
miaka 50 ijayo tutapiga hatua kubwa zaidi. Hivyo, ninaomba kutoa
wito kwa wadau wote wa maendeleo kwamba hatua tuliyopiga ni
nzuri lakini tunatakiwa kuongeza juhudi zaidi katika kutekeleza
mipango
mbalimbali
tuliyonayo
ili
tuweze
kufikia
malengo
yaliyowekwa katika dira ya Taifa ya Mwaka 2025. TUMETHUBUTU
TUMEWEZA NA TUNAZIDI KUSONGA MBELE
Bibi. Gertrude K. Mpaka
Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa
Tarehe 01 Novemba, 2011
viii
SURA YA 1
1.0 HISTORIA FUPI YA MKOA:
1.1
Mahali Mkoa ulipo
Mkoa wa Iringa uko katika Nyanda za Juu za Kusini mwa Tanzania.
Mkoa huu unapakana na ukanda mkavu wa kati wa Tanzania katika
upande wa kaskazini na kupakana kusini na Ziwa Nyasa. Mkoa wa
Iringa umetanda kati ya latitudo 7o 05
longitude 33o 47
hadi 36o 32
na 12o 32
kusini, na
mashariki mwa Meridian. Mkoa wa
Iringa unapakana na Mikoa ya Dodoma na Singida upande wa
kaskazini, Mkoa wa Mbeya upande wa Magharibi, Mkoa wa
Morogoro upande wa Mashariki na Mkoa wa Ruvuma kwa upande
wa kusini. Ziwa Nyasa linatenganisha Mkoa wa Iringa na nchi ya
Malawi upande wa kusini Magharibi mwa Tanzania.
1.2. Eneo la Mkoa
Mkoa wa Iringa una eneo lenye ukubwa wa jumla ya km2
58,936.
Wastani wa asilimia 74 ya eneo hili linafaa kwa shughuli za kilimo
ambalo ni sawa na km2 43,935. Eneo linalobakia la km2 15,001 ni
eneo la maji, hifadhi ya mbuga za wanyama, milima na misitu.
Chati: Mgawanyo wa eneo la Mkoa kiwilaya.
ENEO LA MKOA WA IRINGA
MAKETE
7%
LUDEWA
14%
IRINGA
36%
NJOMBE
18%
KILOLO
13%
MUFINDI
12%
Chanzo: Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa
1
1.3. Utawala
Mkoa wa Iringa umegawanyika katika Wilaya sita ambazo ni Iringa,
Kilolo,
Mufindi,
Njombe,
Makete
na
Ludewa.
Mkoa
pia
umegawanyika katika Halmashauri nane ambazo ni Halmashauri ya
Manipaa Iringa, Halmashauri ya Mji Njombe na Halmashauri za
Wilaya za Iringa, Kilolo, Mufindi, Njombe, Makete na Ludewa. Aidha
Mkoa umegawanyika katika Tarafa 33 Kata 189 na vijiji 736 na
mitaa 206.
Jedwali Na 1: Maeneo ya kiutawala Kiwilaya
Halmashauri
Iringa
Kilolo
Mufindi
Njombe
Makete
Ludewa
Iringa (M)
Mji Njombe
Mkoa
Eneo Km2
Tarafa Kata
20,576
7,882
7,123
10,668
4,128
8,397
162
3,212
62,148
5
3
5
7
6
5
1
1
33
25
22
30
36
22
25
16
13
189
Vijiji
119
106
125
161
97
77
7
44
736
Mitaa
-
-
16
16
-
-
148
26
206
Chanzo: Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa
1.4. Idadi ya watu
Kutokana na matokeo ya Sensa ya kwanza ya Watu na Makazi
iliyofanyika baada ya Uhuru mwaka 1967, Mkoa wa Iringa ulikuwa
na Wakazi 689,905. Matokeo ya Sensa ya mwaka 2002 Mkoa wa
Iringa ulikuwa na watu 1,490,892 kati ya hao wanaume walikuwa
705,743 na wanawake 785,149. Ongezeko la watu kwa mwaka ni
asilimia 1.6. Wilaya ya Njombe ilikuwa inaongoza kwa kuwa na idadi
kubwa ya watu (419,115) wakati Wilaya ya Makete ilikuwa na idadi
ndogo ya watu (105,775). Makadirio ya idadi ya watu mwaka 2011
ni
1,764,285
(me
854,785
2
na
ke
909,500)
Jedwali Na 2: Idadi ya watu kiwilaya mwaka 1967, 1978, 1988, 2002 na 2011
Halmashauri Mwaka
Mwaka Mwaka Makadirio
1978
1967
Mwaka 1988 2002 ya idadi ya watu
watu 2011
Ongezeko
la Wastani wa
kwa watu
kwa
mwaka 1988- km2 (2002)
2002 (%)
Iringa
362,137 245,033 275,457 * 13
x x 204,372 231,198 ** 28
Mufindi 118,467 173,782 229,259 282,071 326,614 1.5 42
Njombe 318,811 236,691 313,991 419,115 501,096 2.1 42
Kilolo
226,124 290,497
x
Makete xx 91,220 102,614 105,775 120,820 0.2 27
Ludewa xx 75,690 100,216 128,155 150,508 1.8 16
26,503 57,164 84,860 106,371 158,592 1.6 700
689,905 925,044 1,193,077 1,490,892 1,764,285 1.6 27
Iringa(M)
Jumla Mkoa
Chanzo: Matokeo ya sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2002.
x: Idadi ya watu imejumuishwa katika Wilaya ya Iringa
xx: Idadi ya watu imejumuishwa katika Wilaya ya Njombe
*Idadi ya watu iligawanywa katika Wilaya ya Iringa na Kilolo
**Mwaka 1988 hapakuwa na Wilaya ya Kilolo
3
1.5 Hali ya hewa
1.5.1 Majira ya mwaka
Majira ya Mkoa wa Iringa hutofautiana kutoka maeneo yenye hali ya
nusu jangwa hadi maeneo ya ubaridi wa Kitropiki. Zaidi ya theluthi
mbili ya Mkoa hupata mvua za kutosha za mtawanyiko kiasi cha
milimita 1,000 kwa mwaka kati ya mwezi Novemba na Mei. Maeneo
yenye mwinuko kati mita 1,200 hadi 2,000 hupata mvua nyingi za
kutosha kiasi cha milimita 1,500 na ukanda wa kati hupata mvua za
wastani.
1.5.2 Hali ya joto
Hali ya joto la Mkoa wa Iringa hutofautiana kutokana na mwinuko;
Ukanda wa chini uliopo Kaskazini mwa Mkoa wa Iringa (Mtera)
hupata joto kiasi cha sentigredi 28 katika mwezi Novemba na
kiwango cha wastani wa nyuzi joto 0o sentigredi, hupatikana katika
safu ya milima ya Kipengere (Kitulo) kati ya mwezi Julai na Agosti.
Tofauti ya majira ya mwaka katika Mkoa inatofautisha hali za
maisha ya watu kutoka eneo moja hadi jingine kutegemeana na
shughuli
wanazozifanya.
imegawanyika
katika
Hali
ya
kanda
hewa
tatu
ya
Mkoa
wa
zinazotofautisha
Iringa
sehemu
mbalimbali. Nyanda hizi ni Nyanda za juu, Nyanda za kati na
Nyanda za chini.
Jedwali: Na. 3:
Hali ya Hewa
Na UKANDA
MWINUKO(Mita)
1 Nyanda za Juu 1600-2700
2 Nyanda za Kati 1200-1600
3 Nyanda
 za 900-1200
Chini
4
MVUA
1000-1600
600-1000
500-600
HALI
YA
JOTO
<15 oC
15-20 oC
20-25 oC
1.5.3. Mvua
Mkoa wa Iringa una msimu mmoja tu wa mvua inayonyesha kati ya
Novemba na Mei. Ukame katika Nyanda zenye mvua nyingi huwa
mfupi zaidi kuanzia mwezi Juni hadi Septemba wakati pepo kavu na
baridi za kusini mashariki (Monsoon) huvuma na wakati huo huwa
ni kiangazi.
1.6 Udongo
Mkoa wa Iringa una aina ya pekee ya maumbo na umeainishwa kwa
kuwa na hali ya hewa ya aina mbalimbali na aina nyingi za udongo.
Kwa mfano mvua ya masika hutofautiana kati ya sehemu na
sehemu, huanzia milimita 500 hadi zaidi ya milimita 1600. Nyanda
za mwinuko/milima ni zenye udongo mwekundu au aina ya njano
mwepesi na rutuba ndogo kutokana na kuchujika na mvua nyingi.
Udongo aina hii wahitaji kurutubishwa mara kwa mara ili kuzalisha
mazao mengi na mazuri. Udongo una upungufu wa madini ya aina
ya calcium, magnesium, Phosphorus na Nitrogen.
1.6.1. Umbile la Ardhi
Sehemu kubwa ya Mkoa wa Iringa ina umbile la mfululizo wa milima
ya Kipengere na Livingstone kwa upande wa kusini; na milima ya
Udzungwa ambayo hutenganisha mikoa ya Iringa na Morogoro.
Sehemu ya Kaskazini ya Mkoa wa Iringa ni tambarare, pia na
sehemu za mwinuko zilizokatishwa na sehemu ya Mashariki ya
Bonde la Ufa ambamo mto Ruaha hupita. Mkoa wa Iringa una
mwinuko wa nchi kutoka usawa wa bahari kati ya mita 500 hadi
kuvuka mita 2000 katika milima ya Kipengere. Pamoja na kuwepo
kwa Bonde la Ufa vile vile kuna uwanda wa juu wenye sehemu
zilizopindika. Uwanda wa juu umechukua sehemu kubwa ya Mkoa,
uwanda
huu
umekatishwa
sehemu
5
nyingi
na
mabonde
ya
miteremko mikali itokanayo na mmomonyoko wa ardhi kwa miaka
mingi tangu nyakati za Jurassic.
1.6.2. Mabonde na Mito
Mkoa wa Iringa ni moja ya chanzo cha mito inayotiririka katika
bahari ya Hindi. Mto Ruaha Mkuu na Ruaha Mdogo huunganika na
Mto Rufiji nje ya Mkoa wa Iringa na kufanya muungano huo kuwa
Bonde la Mto Rufiji. Mtiririko wa maji ya mito hutegemea majira ya
mwaka, huwa mengi wakati wa mvua. Ujenzi wa bwawa la Mtera
katika Wilaya ya Iringa vijijini umefanya bwawa hili kuwa chanzo
muhimu cha umeme kutokana na nguvu ya maji, na hii pia kwa
kiwango kikubwa imebadilisha mtiririko wa maji kuelekea mto
Ruaha Mkuu.
1.7. Shughuli za Kiuchumi
Shughuli kuu za uchumi za Mkoa wa Iringa ni Kilimo, ufugaji,
upasuaji mbao, uvuvi, biashara na ajira za maofisini na viwandani.
Asilimia 85 ya wakazi wa Iringa hujishughulisha na kilimo au kilimo
na ufugaji.
Mazao makuu ya chakula na biashara ambayo yanalimwa ni pamoja
na mahindi, ngano, pareto, chai, viazi mviringo, matunda, alizeti,
karanga, ufuta, maharagwe, nyanya, mpunga, tumbaku, soya,
mtama, mhogo, korosho, Artemesia na paprika. Kati ya mazao yote
yanayozalishwa Mkoani Iringa ni machache tu ndiyo yanayo sindikwa
ndani
ya
Mkoa
huu,
hivyo
huuzwa
yakiwa
ghafi
ambayo
hayajaongezewa thamani. Hii imesababisha kilimo kutowanufaisha
sana wakazi wa Mkoa huu na hivyo kuendelea kuwa na kipato cha
chini.
1.8. Pato la Mkoa wa Iringa
Ingawa Mkoa wa Iringa ni miongoni mwa wazalishaji
wakubwa wa
mazao ya chakula na hasa mahindi na viazi, pato la Mkoa
6
kwa
mwaka 1961 lilikuwa ni Sh. 5,693,000 na Wastani wa pato la mtu
kwa mwaka lilikuwa ni Sh. 103. Aidha, pato la Mkoa kwa mwaka
2010 lilikuwa Sh. 1,702,430,000 na pato la mkazi lilikuwa Sh.
979,882.
Hata hivyo, pato hili la Mkoa huchangiwa kwa kiasi kikubwa na
mashamba makubwa ya tumbaku, chai, viwanda vya chai, misitu na
viwanda vya mbao.
7
SURA YA 2.
2.0: MUUNDO WA MKOA ULIVYOBADILIKA
NYAKATI TOFAUTI KUANZIA 1961
KATIKA
Mkoa wa Iringa ulianzishwa Mwaka 1964 kutoka Mkoa wa zamani
ambao uliitwa Jimbo la Kusini la Nyanda za Juu. Makao Makuu
yakiwa Mbeya. Mkoa ulikuwa na Wilaya mbili ambazo ni Njombe na
Iringa. Wilaya ya Mufindi ilianzishwa Mwaka 1964, Wilaya ya
Ludewa Mwaka 1975, Makete Mwaka 1979 na Kilolo Mwaka 2002.
Hadi kufikia Mwaka 1975 Mkoa ulikuwa na Wilaya nne ambazo ni
Iringa, Njombe, Ludewa na Mufindi. Kuanzia hapo hadi 2011 Mkoa
una Wilaya sita ambazo ni Iringa, Kilolo, Mufindi, Njombe, Ludewa
na Makete. Mkoa unatarajiwa kugawanyika kuwa Mikoa miwili ya
Iringa na Njombe kuanzia Julai, 2011.
Kufikia Mwaka 1968,Mkoa ulikuwa na Halmashauri za Wilaya tatu
ambazo ni Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Halmashauri ya Wilaya
ya Njombe na Halmashauri ya Mji wa Iringa. Ingawa Wilaya ya
Mufindi ilikuwa imeanza Mwaka 1964 haikuwa na Halmashauri yake
(Wilaya iliendelea kutumia Halmashauri ya Wilaya ya Iringa). Hivi
sasa Mkoa una Halmashauri nane ( Halmashauri ya Manispaa ya
Iringa, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Halmashauri ya Wilaya ya
Kilolo, Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, Halmashauri ya Wilaya ya
Makete, Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Halmashauri ya Wilaya
ya Njombe na Halmashauri ya Mji wa Njombe.
2.1 Madaraka Mikoani:
Umuhimu wa kuwashirikisha wananchi katika kuamua mambo yao
wenyewe ulitiwa katika vitendo mwaka 1972 wakati Mpango wa
Madaraka Mikoani
27/1972
(THE
ulipotekelezwa.
Serikali
DECENTRALISATION
8
kupitia
OF
Sheria Na.
GOVERNMENT
ADMINISTRATION
(INTERIM
PROVISIONS)
ACT,
1972)
ilianzisha Madaraka Mikoani kwa lengo la kupeleka Madaraka
Mikoani ilikuwa ni kusogeza huduma karibu na wananchi na
kuharakisha Maendeleo katika Mikoa.
2.2 Vijiji na Madaraka Vijijini:
Baada ya Uhuru Serikali iliweka pia nguvu katika kuanzisha vijiji kwa
ajili ya kuharakisha Maendeleo ya watu. Tarehe 12 Agosti, 1975
Serikali ilianzisha Sheria iliyotaka wananchi kuishi vijijini. Mwaka
1975 Mkoa wa Iringa ulikuwa na Jumla ya Vijiji 467 vyenye Jumla ya
Kaya 181, 308.
Jedwari Na 4:Linaonyesha idadi ya Vijiji na kaya kwa Mwaka 1975
WILAYA IDADI YA VIJIJI KAYA
Iringa 149 53,437
Njombe 154 69,586
Mufindi 117 40,058
Ludewa 47 18,227
Jumla 467 181,308
Chanzo: Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.
Mpango huu wa watu kuishi pamoja vijijini umekuwa ndio chimbuko
(Nucleus) kuu la umoja, amani na Maendeleo ya kiuchumi ambayo
Mkoa wa Iringa unajivunia.
9
2.3: Sekretarieti za Mikoa:
Sekretarieti zilianzishwa kwa Sheria Na. 19 ya Mwaka 1997.
Madhumuni ikiwa ni kusimamia utekelezaji wa Sera za Serikali na
kuhakikisha kuwa watekelezaji mbalimbali wanazingatia maelekezo
ya Serikali kwamba malengo yaliyowekwa na Taifa yanafikiwa.
Serikali za Mitaa chini ya Halmashauri za Miji na Wilaya zina jukumu
la kusimamia shughuli za uzalishaji mali, huduma za kiuchumi na
kijamii katika maeneo yao.
2.4: Hali ya Uongozi na Utawala kuanzia 1961;
Mkuu wa Mkoa wa kwanza wa Iringa baada ya Uhuru ambaye
alikuwa pia ni Katibu wa TANU wa Mkoa alikuwa ni Mhe. Phillemon
P. Muro. Mhe. Phillemon Muro aliwahi pia kuwa Balozi wa Tanzania
nchini Sweden. Majedwali yafuatayo yanaonyesha orodha ya Wakuu
wa Mikoa na Wakurugenzi/Makatibu Tawala wa Mkoa waliowahi
kuongoza Mkoa wa Iringa kwa vipindi tofauti:
Jedwali 5: Wakuu wa Mikoa Iringa.
NA JINA KAMILI MWAKA
1 Mhe. Phillemon P. Muro 1964 1965
2 Mhe. Said S. Chamshama 1965 1968
3 Mhe. John B. Mwakangale 1968 1970
4 Mhe. Dr. Wilbert Kleruu 1970 1971
5 Mhe. Mohamed M. Kissoky 1971 1977
6 Mhe. Shaidi A. Kabongo 1977 1986
7 Mhe. Samwel J. Sitta 1986 1987
8 Mhe. John S. Malecela 1987 1988
9 Mhe. Col. (Mstaafu) Anatoli Tarimo 1988 1991
10 Mhe. Maj.Gen. (Mst.), Herman Lupogo 1991 1993
10
11 Mhe. Marcel B. Komanya 1993
1995
12 Mhe. Joseph J. Mungai 1995
1996
13 Mhe. Nicodemus M. Banduka 1996
1998
14 Mhe. Njelu M. Kassaka 1998
1999
15 Mhe.Maj. Gen. (Mst), James E. Luhanga 1999
2006
16 Mhe. Capt (Mst) Jaka Mwambi 2006 - 2006
17 Mhe. Halima Y. Kasungu 2006-2007
18 Mhe. Hajjat Amina M. Said 2007
2009
19 Mhe. Mohamed Abdulaziz (MB) 2009
2010
20 Mhe. Dr. Christine G. Ishengoma (MB) 2011-Mpaka sasa
Jedwali
Na
6:
Makatibu
Tawala
na
Wakurugenzi
wa
Maendeleo wa Mkoa wa Iringa kwa kipindi cha 1961 hadi
2011
NA JINA KAMILI MWAKA
1. Bw. S. K. Musyani 1961-1964
2. Bw. A. Suleiman 1964 1965
3. Bw. Y. Semhando 1965 1967
4. Bw. S F. Mkumbukwa 1965- 1967
5. Bw. M. J. Mbelwa 1967 1972
6. Bw. Hussein R. Shekilango 1972 1974
7. Bw. Horace Kolimba 1974 1975
8. Bw. Hosea Z. Talawa 1975 1979
9. Bw. James F. Gwagilo 1979 1982
10. Bw. Emilli Mudogo 1984 1989
11. Bw. Julius Matiko 1989 1993
12. Bw. Charles Keenja 1993 1995
11
13. Bw. Fred Mwaisaka 1995
1997
14. Bibi. Cecilia Shirima 1997
2006
15. Bw. Bernard Nzungu 2006
2008
16. Bibi. Gertrude K. Mpaka 2008 hadi sasa
Chanzo: Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa
12
2.5: Viongozi wa sasa wa mkoa wa Iringa
MKUU WA MKOA
MHE. DR. CHRISTINE
G. ISHENGOMA (MB)
KATIBU TAWALA WA
MKOA
BIBI. GERTRUDE K.
MPAKA
MAKATIBU TAWALA WASAIDIZI WA MKOA
Sehemu ya Sehemu ya Mipango
Rasilimali Watu na Uratibu
Bw. Barnabas Bw. Nuhu
Ndunguru Mwasumilwe
Sehemu ya
Miundombinu
Sehemu ya Sehemu ya Uchumi
Serikali za Mitaa na Uzalishaji
Dr. Ezekiel
Mpuya
Bw. Vicent.
James
Sehemu ya Bibi. Wamoja Bw. Adam Swai
Huduma za Jamii Ayubu
WAKUU WA WILAYA
Mkuu wa Wilaya ya
Iringa
Mhe. Capt Aseri
Msangi
Mkuu wa Wilaya Mkuu wa Wilaya Mkuu wa Wilaya Mkuu wa wilaya ya
ya Njombe ya Makete ya Ludewa Mufindi
Mhe. Sarah Mhe.Zainabu Mhe. Georgina Mhe. Evarista
Dumba Kukwega Bundala Kalalu
13
SURA YA 3.
3.0: MAJUKUMU NA MALENGO YA MKOA
3.1:
Dira ya Mkoa
Mkoa ni Taasisi ya Umma inayowezesha na kusimamia utekelezaji
wa Sera, Sheria, Kanuni na Miongozo mbalimbali ya Serikali kwa
wakati na ufanisi wa hali ya juu.
3.2: Dhamira ya Mkoa
Kuwa Taasisi yenye
unaotosheleza
kutoa
wataalamu
huduma
za
wenye
ushauri
uwezo
na
na
ujuzi
utaalamu
kwa
kushirikiana na Wadau wengine wa Maendeleo kwa kuzingatia Sera,
Sheria, na Miongozo ya Serikali ili kutoa huduma bora kwa
wananchi.
3.3: Majukumu ya Mkoa
· Kuziwezesha na kuzijengea uwezo Mamlaka za Serikali za Mitaa
ili ziweze kutoa huduma zinazohitajika kwa wananchi
·
Kuhakikisha huduma bora za kiuchumi na kijamii zinawafikia
Wananchi walio wengi kwa ubora na viwango vinavyostahili
·
Kuhakikisha
amani,
usalama
na
mshikamano
unakuwepo
Mkoani kwa kuzingatia Utawala Bora
·
Kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa Mpango wa Kukuza
Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (MKUKUTA)
·
Kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa Mipango ya Elimu
(MEM, MES), Mpango wa kuendeleza kilimo (ASDP/DADP),
Mpango wa Afya na utekelezaji wa miradi yote ya Maendeleo
·
Kuhakikisha masuala mtambuka (Ukimwi, Mazingira, Jinsia, nk)
yanapewa vipaumbele vinavyostahiki wakati wa kuandaa na
kutekeleza Mipango ya Maendeleo.
14
3.4: Mikakati ya Mkoa
Katika kipindi cha miaka mitano kuanzia 1961 hadi
2010,
Serikali ilipanga kutekeleza malengo na mikakati mbalimbali
ili kuondoa kero na kuboresha maisha ya Watanzania.
3.4.1 Mikakati hiyo ni pamoja na kutekeleza:-
· Ilani ya Uchaguzi ya TANU/ CCM ya mwaka 1961 hadi 2010
· Mkakati wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Miaka
Mitano na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, chini ya utaratibu
wa mpango wa matumizi wa muda wa kati (MTEF).
·
Mkakati
wa
kukuza
uchumi
na
kupunguza
umaskini
(MKUKUTA).
· Matakwa ya Sera na Sheria zinazosimamia Sekta mbalimbali.
· Mkakati wa kitaifa wa Kupambana na Kuzuia Rushwa.
· Sera ya Taifa ya kupambana na UKIMWI.
· Utekelezaji wa Malengo ya Millinia 2005
2010
3.4.2: Katika kuhakikisha mafanikio yanapatikana Mkoa ulijiwekea
mikakati ifuatayo:-
a)
Kuweka mazingira mazuri ya kufanyia kazi yenye ufanisi
mkubwa ili kutoa huduma bora kwa wananchi.
b)
Kutengeneza mazingira bora ya Utawala kwa kudumisha
amani na umoja.
c)
Kutoa huduma kwa wananchi kwa kuwapatia ushauri wa
kitaalamu.
d)
Kuhakikisha tunaongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali ya
chakula na biashara, kuongeza ubora wa mazao na kuuza
kwa bei nzuri na hatimaye kuongeza kipato na pato la
Mkoa na Taifa kwa ujumla.
e)
Kuhakikisha wadau mbalimbali wanashiriki katika shughuli
za Maendeleo.
f)
Kuandaa Mipango shirikishi na endelevu.
15
g)
Kuweka mikakati madhubuti ya mapambano dhidi ya
maambukizi ya virusi vya UKIMWI na UKIMWI.
16
SURAYA 4.
4.0: MABADILIKO NA MATUKIO MAKUU KATIKA MFUMO WA
KISIASA, KIULINZI, KIUTAWALA, KIUCHUMI, KITEKNOLOJIA
NA KIJAMII
4.1: Mafanikio yaliyopatikana hadi sasa
4.1.1 Pato la Mkoa:
Pato la Mkoa mwaka 1961 lilikuwa ni Sh.5,693,000 wakati
pato la Mkazi lilikuwa Sh.
103, Mwaka 2010 pato la Mkoa
limefikia Sh. 1,702,430,000,000 na pato la Mkazi lilikuwa
limeongeka kufikia Sh. 979,882 sawa na ongezeko la Sh.
979,779. Jedwali lifuatalo linaonyesha ukuaji wa pato la
Mkoa na pato la Mkazi kutoka mwaka 1961 hadi 2010
Jedwali Na. 7: Pato la Mkoa kipindi cha 1961 hadi 2010:
Mwaka
Pato la Mkoa (Sh)
Pato la Mkazi (Sh)
1961
5,693,000
103
1995
92,021,000
102,570
2009
1,469,720,000,000
859,875
2010
1,702,430,000,000
979,882
Chanzo: Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).
4.1.2 Ukusanyaji wa Mapato
Katika kipindi cha 1961/62 hadi 2010/11 Mamlaka ya Mapato
Tanzania iliendelea na ukusanyaji wa Mapato kutokana na kodi ya
mapato, Kodi ya ongezeko la thamani na ushuru wa forodha.
Jedwali Na. 8: Makadirio na Makusanyo ya Kodi kwa kipindi
cha 1961/62 hadi 2010/11
Mwaka
Makadirio Makusanyo
(Sh)
Asilimia
(Sh)
1961/62 10,000,000 9,952,938 99
1997/98 89,000,000 128,702,105.50 144
2009/10
8,441,500,000
8,677,477,835
Chanzo: Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Iringa
17
103
4.1.3 Mapato toka Serikali Kuu.
Katika kipindi cha 1961/62 hadi 2010/11 Mkoa na Halmashauri za
Wilaya zimeendelea kupokea fedha kutoka Serikali kuu na Wahisani
mbalimbali ikiwa ni pamoja na fidia kutoka vyanzo mbalimbali
vilivyofutwa kwa utekelezaji wa miradi ya Maendeleo. Jedwali
lifuatalo linaonyesha mapokezi ya fedha kwa ajili ya miradi ya
Maendeleo.
Jedwali Na. 9: Mapato kutoka Serikali Kuu
Mwaka
Chanzo
Kiasi idhinishwa Kiasi
(Sh) (Sh)
1961/62
Serikali Kuu
1,666,920
Wafadhli
531,450
Jumla
2,198,370
1990/91 Serikali Kuu
1,482,000,000
Wafadhili
4,118,000,000
Jumla
5,600,000,000
2009/10 Serikali Kuu
7,762,436,000
Wafadhili
21,542,446,551
Jumla
29,304,882,551
Chanzo: Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
kilichotolewa Asilimia
1,666,920
531,450
2,198,370
1,482,000,000
4,118,000,000
5,600,000,000
5,739,844,000
21,813,085,180
27,552,929,180
4.1.4 Mapato ya Halmashauri:
Katika ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kumekuwa na
ongezeko la Sh. 5,160,049,889 sawa na asilimia 300 ikilinganishwa
na mapato ya Sh. 1,646,889 ya mwaka 1961/62. Kuanzia kipindi
cha 1961/62 hadi 2010/11 Halmashauri za Wilaya zimeweza
kusimamia kikamilifu makusanyo ya mapato yake ya ndani kama
ilivyoainishwa katika jedwali lifuatalo:
Jedwali Na. 10: Mapato ya Halmashauri za Wilaya
Mwaka
Mapato
Makisio (Sh)
Halisi (Sh)
18
Asilimia
100
100
100
100
100
73
101
94
1961/62 1,656,920 1,646,889 99
1989/90 167,089,200 102,437,630 61
2010/11 7,325,163,015 5,160,049,889 70
Chanzo: Ofisi ya Mkuu wa Mkoa (Takwimu za 1961/62 ni za
Halmashauri tatu za Iringa,Njombe na Mji wa Iringa).
4.2 Utawala Bora
· Rejesta na masanduku ya maoni yamewekwa katika sehemu
zote za kutolea huduma ili kuboresha utoaji wa huduma.
·
Mbinu Shirikishi ya Fursa na Vikwazo vya Maendeleo (O & OD)
na inayowahusisha wadau wengine wa Maendeleo hutumika
katika kupanga Mipango ya Maendeleo kuanzia ngazi ya kijiji
·
Ongezeko la njia/vyombo vya mawasiliano (Radio mbalimbali
za Umma, binafsi, Madhehebu ya dini, Mashirika ya simu ya
Umma na binafsi)
hadi vijijini. Kuboresha mazingira ya
kufanyia kazi ikiwa ni pamoja na vyombo vya usafiri na Ofisi
kwa watendaji na wataalamu wa sekta mbalimbali. Ofisi 14 za
Maafisa Tarafa wa Mahenge, Malangali, Ikuwo, Ukwama,
Magoma,
Makambako,
Kibengu,
Ifwagi,
Mlolo,
Kalenga,
Masasi, Mwambao, Liganga na Pawaga zimejengwa na Ofisi 1
ya Iringa Mjini imefanyiwa ukarabati.
19
Picha ya Juu ni Ofisi ya zamani ya Afisa Tarafa wa Kibengu Wilaya ya Mufindi
iliyojengwa Mwaka 1953;Chini ni Ofisi Mpya ya Tarafa ya Kibengu.
·
Kumekuwepo na uzingatiaji jinsia katika masuala ya ajira na
utumishi kwenye Halmashauri na Mkoa.
·
Miundo ya Kamati za Halmashauri imezingatia mahitaji
20
·
Pamekuwepo na uhuishaji wa takwimu za sekta zote ili kupata
picha ya hali halisi ilivyo.
·
Ongezeko la ukusanyaji mapato ambayo yanatuwezesha
kuendelea kujitegemea kama taifa
kwa Mipango yetu ya
Maendeleo.
4.3 Utekelezaji wa Mipango na Bajeti
Kwa ujumla kumekuwa na ongezeko
la
bajeti
kwa
fedha
zilizotengwa na zilizopokelewa ukilinganisha kipindi cha 1961
na
2010. Mwaka 1961/62 Mkoa na Halmashauri zake ulitengewa jumla
ya shilingi(kwa miradi ya Maendeleo. Fedha za ndani na nje)
2,198,370 na zikapokelewa Sh. 2,198,370( 100 %).Mwaka 2009/10
Mkoa ulitengewa jumla ya Sh. 29,304,882,551 na zilipokelewa Sh.
27,552,929,180 (94 %).
4.4. Huduma za kiuchumi
4.4.1 Kilimo
Mkoa una jumla ya eneo la hekta 58,936,000 kati ya hizo km za
mraba 56,864 ni nchi kavu na km za mraba 2,072 ni eneo la maji.
Kati ya eneo lote hekta
43,935,000 (74%) linafaa kwa kilimo
ingawa hekta zinazotumika kwa kilimo hadi sasa ni 7,468,950 tu;
sawa na asilimia 17.
Mazao makuu ya chakula na biashara ambayo yanalimwa ni pamoja
na Mahindi, Ngano, Pareto, Chai, Viazi mviringo, Matunda, Alizeti,
Karanga, Ufuta, Maharagwe, Nyanya, Mpunga, Tumbaku, Soya,
Mtama, Mhogo, Korosho.
21
Uzalishaji wa Mahindi Wilayani Njombe
Uzalishaji wa Chai Shamba la Kibena Wilayani Njombe
Eneo linalolimwa mazao mbalimbali limeongezeka kutoka Hekta
305,208.65 mwaka 1961/62 hadi kufikia Hekta 858, 838 zilizolimwa
22
msimu 2010/11. Elimu ya kilimo bora ilitolewa kwa wakulima na
jumla ya mashamba darasa 1,603 yalianzishwa na jumla ya wakulima
49,075 wamepatiwa mafunzo kwa vitendo kupitia mashamba haya
kwa kipindi cha 1961 hadi 2010.Pia ili kufikisha Elimu kwa Wakulima
waliowengi Mkoa umeanzisha vituo vya rasilimali watu wa Kilimo
katika Kata 17 (WARC) Ward Agricutural Resources Centres.
Mbolea zilizotumika mwaka 1961/62 zilikuwa tani 16,826 na tani 300
za mbegu. Ukilinganisha na tani 45,647 za mbolea na tani 3,615 za
mbegu mwaka 2010 hii ni sawa na ongezeko la asilimia 63.1 kwa
matumizi ya mbolea..
Jedwali Na. 11:
Uzalishaji wa Mazao Makuu ya Chakula na
Biashara 1961/62 hadi 2010/11
Zao
1961/62
1995/96
2010/11
Hekta Hekta Mavuno Hekta Mavuno
limwa
Mahindi
Mavuno (Tani) limwa (Tani) limwa (Tani)
103,254 112,381 250,520 385,799 433,865 967,932
4,622 7,137 40,456 6,580 98,079 100,522
14,654 15,431 22,008 79,844 37,609 182,957
Muhogo 417 579 723 1,023 2,804 2,699
Mpunga 3,213 4,305 7,823 6,423 17,478 42,255
Ngano 8,134 932 13,611 17,169 15,620 22,798
Tumbaku 3,215 2,134 475 1,400 1,882 1,566
Chai 4,551 4,517 6,289 7,678 16,789 47,558
Pareto 259 248 4,523 1,818 1,884 310
Alizeti 712 891 10,203 7,805 67,979 70,429
Kahawa 891 712 1,254 71 1,387 191
143,922 149,267 357,885 515,610 695,376 1,439,217
Maharage
V/Mviringo
JUMLA
Chanzo: Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa
23
4.4.2 Mifugo
Mkoa una jumla
ya
mashamba
yanayomilikiwa na serikali
makubwa
ya
mifugo
na watu binafsi. Mashamba
27
haya
huzalisha maziwa, mitamba na madume. Madume haya hutumiwa
zaidi na wakulima wadogo kuboresha mifugo yao.
Ufugaji wa Ngo mbe wa Maziwa Shamba la Kibebe Wilaya ya Iringa
Ufugaji wa kuku wa kienyeji Wilayani Ludewa
24
Jedwali Na. 12: Takwimu za sekta ya mifugo kwa kipindi cha
1961 hadi 2010:-
Takwimu/ Desemba Desemba Desemba ONGEZEKO/
Huduma 1961 1995 2010 MAFANIKIO
9,176 480,410 568,749 Idadi
Idadi ya
ng ombe wa
ya
ng ombe
kienyeji
imeongezeka
kwa
24
%.
Wafugaji
wanazingatia
ufugaji wa
kibiashara na
ubora wake na
siyo wingi wake
Idadi ya
19
1,790
28,081
Idadi
ng ombe wa imeongezeka
maziwa na kwa 99%
nyama(kisasa)
Miundo mbinu
Majosho Yaliyokuwepo Majosho Majosho
yaliyokuwepo-69 156. yaliyopo- 226 yanayofanyakaz
yaliyokarabatiwa Yaliyokarabati yaliyokarabatiw i yameongezeka
22 wa a 93 hadi kufikia 161
yaliyotumika 58 yaliyotumika yanayotumika sawa na 63.9%
117 161 ongezeko
40
na
hili
kubwa ni baada
ya
serikali
kusambaza
dawa ya ruzuku.
Uzalishaji wa Maziwa
maziwa na
lt
4,040,000
1,592,662
Maziwa
lt
6,976,018.
Lita
5,383,356
ikiwa ongozeko
nyama
Nyama
68,123
Jumla
ya
Nyama
ya
mifugo(ngombe, mifugo(ngombe,
kondoo, mbuzi na kondoo,
nguruwe) na
walichinjwa
mbuzi
nguruwe)
72,634
25
la
77.2%
Jumla
22,102
ni
Ng ombe 16,568
walichinjwa
Kondoo/mbuzi
25,923
2,970
Ng ombe
26,379
Nguruwe 2,564.
19,348
Kondoo/Mbuzi
22,008
22,318
Nguruwe
24,247
Uogeshaji
Idadi ya miruko
1,314,158
Ongezeko
Ng ombe
Ng ombe 802,220
Idadi ya miruko miruko
1,
1,513,056.
ngombe
la
kwa
ni
88.6%.
Mbuzi 107,133
Mbuzi 404,024.
302,118
Kondoo 71,372
Kondoo 135,121
Mbwa 10,728 Mbwa 26,728 Vipande
Zao la ngozi
98,121 17,128 Vipande 18,375 Ongezeka
vya 20.7%
vya
14,568
ngozi
ya
ngozi
ya
ng ombe viliuzwa. ngombe Vipande 2,820 vya viliuzwa. Ongezeko
Vipande 17,970 84.5%
ngozi
ya
14,825
Kondoo/Mbuzi vya
ngozi
viliuzwa.
ya
Kondoo/Mbuzi
viliuzwa.
Uboreshaji
wa
Chanjo ya mdondo
925,319
Kuku Ongezeko
waliochanjwa kuku 1,057,413
kuku waliochanjwa kuzuia mdondo sawa na asilimia
ni 200,000 ni 1,257,413. 84 hii ni
ufugaji wa kuku
wa
kisasa
kienyeji
na
ni
kwa
sababu ya
matumizi ya
dawa ya matone
ya I2 sanjari na
kampeni
chanjo
kuku
kienyeji
Chanzo: Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa
26
ya
kwa
wa
4.4.3 Uvuvi
Kwa kipindi cha 1961 hadi 2010 jumla ya maeneo yaliyoainishwa
ambayo ni maarufu kwa uvuvi Mkoani ni bwawa la Mtera,
Itombolelo, Ngwazi, Nzivi na Ziwa Nyasa. Uvuvi unafanyika zaidi
katika Ziwa Nyasa ambalo kwa upande wa Tanzania lina ufuko wa
urefu wa km. 260 na mabwawa madogomadogo ya kufugia samaki
4,167. Maeneo haya ya uvuvi yana jumla ya kilomita za mraba 822
ambazo zimezalisha jumla ya Kg. 1, 449,778 za samaki zenye
thamani ya Sh. 4,343,334,000.
Ufugaji shirikishi wa Samaki Wilayani Ludewa
4.4.4 Sekta ya Ushirika
Mkoa una jumla ya Vyama vya Ushirika hai 371 vyenye wanachama
55,764. Kati ya vyama hivi; Vyama vya Mazao ni 134, Vyama vya
Akiba na Mikopo 202, Ushirika wa Maduka ni 5, Vyama vya Viwanda
ni 8, Vyama vya Uvuvi ni 4, Chama cha Madini ni 1, chama cha
mifugo ni 1 vyama vya huduma ni 2, vyama vya nyumba ni 3,
vyama vya umwagiliaji ni 2 Ubia ni1 na Vyama Vikuu ni 2 na
vingine 6. Vyama hivi kwa pamoja vina mtaji wa ndani Sh.
27
2,525,708,130 na vimetoa kwa wanachama wake mikopo yenye
thamani ya Sh. 32,545,782,744.
Jedwali Na. 13: Mafanikio ya sekta ya Ushirika kuanzia 1961
hadi 2010 .
1
Desemba
Maelezo
Vyama
Desemba
1961
Na.
1995
Desemba 2010
Ongezeko
vya 2 186 371 369
ya 460 11,848 55764 55,304
1,620,000 211,350,203 2,525,708,130 2,524,088,130
857,420.20 145,254,201 32,545,782,744 32,391,528,543
- 589,638,500 35,071,547,009 9,976,361,500
Ushirika
2
Idadi
Wanachama
3
Mtaji
wa
ndani (Sh)
4
Mikopo
iliyotolewa
(Sh)
5
Mikopo toka
nje
(Mabenki na
Taasisi)- Sh.
Chanzo: Taarifa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa
4.4.5. Sekta ya Viwanda na Biashara
Sekta ya Viwanda na Biashara, inaajiri watu takriban 50,000 hii
ikiwa ni sawa na
Iringa.
asilimia 2.8 ya wakazi 1,764,285 wa Mkoa wa
Mkoa unazo fursa nyingi zinazoweza kuugeuza Mkoa huu
kuwa wa viwanda, na kuongeza ajira na pia pato la Mkoa. Nia ya
Mkoa ni kuhakikisha sehemu kubwa ya mazao yanayolimwa,
yanasindikwa na kuyaongezea thamani
ili kuinua kipato cha
wazalishaji.
Mkoa kwa hadi sasa unavyo viwanda vya usindikaji 04 vikubwa, vya
kati 53., na vidogo 53, na mashine za kusaga nafaka1,192.
28
Kiwanda kidogo cha kusindika mafuta ya Alizeti Wilayani Mufindi
Jedwali
Na.
14:
Idadi
ya
Wajasiriamali
wadogo
waliowezeshwa mafunzo na mitaji
Eneo
1961/62 1995/96 2010/11
633 2,394 53
Uendeshaji biashara 1,386 9,253 478
Ushauri 4,947 53,971 3,218
Masoko 1,194 4,890 147
Jumla 8,160 70,508 3,896
Usindikaji vyakula
Chanzo; Ofisi ya MKuu wa Mkoa.
Mkoa una jumla jumla ya masoko 43 (2010) ikilinganishwa na
masoko 2 kuanzia 1961 ikiwa ni ongezeko la asilimia 95 Lengo la
Mkoa ni kuwa na soko kwenye kila kata.
29
Mkoa umetenga eneo la ekari 500 katika Halmashauri ya Wilaya ya
kilolo
kwaajili
ya
Export
Processing
Zone
(EPZ)
na
kila
Halmashauri imetenga maeneo kwa ajili ya ujenzi wa Viwanda,
Masoko na Maghala kama ifuatavyo:-
Mufindi
Ekari 100, Ludewa
Ekari 52,156 na Njombe Mji
Ekari
110.
4.4.6. Maliasili
Mkoa
una fursa nyingi za kutumia na kuendeleza maliasili.
Miongoni mwa fursa hizo ni Ufugaji wa nyuki, wanyamapori, Ruaha
National Parks, Kitulo National Park, Udzungwa National Park,
Mpanga/Kipengere Game Reserves, Milima na misitu ya Udzungwa,
Misitu mikubwa ya kupandwa kama msitu wa Taifa wa Sao Hill,
misitu ya kupandwa ya watu binafsi na makampuni yaliyowekeza
katika misitu mfano Green Resource, Halmashauri za Wilaya, misitu
ya asili ya Serikali za Vijiji na Serikali Kuu.
Uhifadhi wa vyanzo vya Maji
Hadi kufikia 2010 jumla ya vyanzo vya maji 5,989 vilikuwa
vimetambuliwa na jumla ya vyanzo 5,989 vimehifadhiwa.
Chanzo cha Maji kilichohifadhiwa Wilayani Njombe
30
4.4.7 Misitu
Jedwali Na. 15: Upandaji wa miti kiwilaya kipindi cha
kuanzia
mwaka
1961/1964
hadi
2010/2011
ni
kama
ifuatavyo:
Wilaya
1961/62
1995/96
Lengo
Halisi
2010/11
Lengo
Halisi
Lengo
Halisi
Makete 0 0 5,000,000 5,759,176 5,000,000 7,518,071
Mufindi 1,000,000 890,800 8,000,000 9,698,664 30,000,000 22,950,200
Kilolo 0 0 0 0 12,000,000 8,351,863
Ludewa 0 0 4,000,000 3,929,468 1,500,000 3,014,320
Njombe 2,000,000 1,685,403 5,000,000 5,759,196 5,000,000 5,709,390
Iringa 1,000,000 931,599 5,000,000 508,618 500,000 508,618
JUMLA 4,000,000 3,507,802 27,000,000 25,655,122 54,000,000 48,052,462
Chanzo: Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Shamba la Miti ya kupandwa Halmashauri ya Mji Njombe
31
Jedwali Na. 16: Ukusanyaji wa Mapato ya Misitu kwa Msimu
wa 1961/62 hadi 2010/11 na Malengo Kiwilaya.
MKOA
Lengo
Halisi
Lengo
Halisi
Lengo
Halisi
/WILAY
A
1961/62
Maliasili
10,000
1995/96
6,850
2010/11
2,000,000
1,668,110
6,000,000
12,200,000
Mkoa.
Iringa
65,000 6,850 15,000,000 12,000,000 27,000,0000 25,980,000
Mufindi 250,000 58,503 150,000,000 178,000,000 350,000,000 412,000,000
Njombe 225,000 416,810 75,000,000 82,000,000 275,000,000 250,000,000
Ludewa 0 0 16,000,000 12,800,000 30,000,000 25,000,0000
Makete 0 0 18,000,000 15,000,000 50,000,000 46,000,000
Kilolo 0 0 0 0 65,000,000 52,000,000
Jumla 550,000 489,013 276,000,000 301,468,110 1,046,000,000 1,048,180,000
Chanzo: Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa
Uwekezaji katika Sekta ya misitu
unakua kwa kasi ya kuridhisha
kutokana na makampuni kutoka nje na ndani kuvutiwa kuwekeza
katika Sekta hii. Hadi mwaka 2010 kulikuwa na makampuni 5
yaliyowekeza katika Sekta ya misitu Wilaya ya Mufindi . Makampuni
hayo ni Mufindi Paper Mills,Mufindi Tea Company,Uniliver Tea
(T),Green Resource na Highland Plantation.
4.4.8 Utalii
Katika kipindi cha 1961 hadi 2010, Mkoa umeainisha vivutio vya
Utalii na unaendelea na zoezi hili kwa kushirikiana na wadau
mbalimbali. Pia Mkoa unaendelea na mchakato wa
kutangaza
vivutio hivyo kwa wawekezaji wa ndani na wa nje ili vivutio hivyo
viweze kutusaidia kupunguza umasikini na kuchangia ukuaji wa
uchumi na Maendeleo ya watu kwa ujumla. Zaidi ya hapo Mkoa
32
unaendelea kuvutia wawekezaji kuboresha miundombinu ya Utalii
ikiwemo ujenzi wa Hoteli ya Kitalii yenye hadhi ya nyota tano katika
Manispaa ya Iringa. Jumla ya vivutio 45 vilikuwa vimetambuliwa
hadi kufikia 2010.
Minara ya Kumbukumbu ya Uhuru ya Mjini Iringa ni kivutio kizuri cha
Utalii.
Maporomoko ya Maji katika kijiji cha kimani Wilaya ya Makete.
33
Picha ya Twiga katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha Mkoani Iringa.
Mafanikio ya Utalii katika Mkoa wa Iringa
Mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya Utalii Mkoa wa Iringa
kuanzia kipindi cha 1961 hadi 2010 ni pamoja na:-
· Kuwepo kwa Maafisa Utalii katika Halmashauri zote 8,
· Mkoa umetengeneza Programu ya ukusanyaji takwimu za
watalii,
· Kuongezeka kwa watalii waliotembelea vivutio mbalimbali,
· Kuongezeka kwa Wawekezaji katika eneo la Utalii,
· Wananchi wa ndani wamehamasishwa kutembelea vivutio hivi
kwa lengo hasa la kuendeleza utalii wa ndani.
·
Halmashauri zimeanzisha mpango mkakati wa masuala ya
uendelezaji utalii na kuanzishwa kwa mabaraza ya biashara
na kikundi cha uendelezajki utalii.
34
·
Kutangaza vivutio vya utalii katika redio, magazeti na kugawa
vipeperushi katika hafla za kitaifa na kikanda kama vile nane
nane.
Jedwali Na. 17: Mafanikio ya Utalii yanaonekana kama
ifuatavyo:-
Sekta
Desemba
Idadi
Desemba Desemba Mafanikio/
1961
Utalii
Shughuli
1995 2010 Ongezeko
ya 750 13,727 17,200 3,473
wa 28 6,747 10,580 3,833
- - 8 8
watalii nje
Watalii
ndani
Maafisa utalii
Chanzo: Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa
4.5. Huduma za Jamii
4.5.1. Elimu
Elimu ya Awali
Kwa kipindi cha 1961 hadi 2010 yamepatikana mafanikio yafuatayo:
·
Kuongezeka kwa madarasa ya awali toka 67 hadi 839 sawa na
ongezeko la asilimia 1,152.
·
Kuongezeka kwa wanafunzi toka 3,015 Hadi 43,075 ambalo ni
ongezeko la asilimia 69.
Jedwali Na. 18: Elimu ya Msingi
JINA LA WILAYA
IDADI YA SHULE
1961/62
1995/96
2010/2011
IRINGA 70 217 188
KILOLO * * 108
LUDEWA * 77 102
MAKETE * 87 97
MUFINDI * 138 172
35
NJOMBE
90 258
160
JUMLA
205 724 925
NB. * Wilaya za Kilolo, Ludewa, Makete na Mufindi zilikuwa bado kuanzishwa.
Mafanikio ya kitaaluma kwa Elimu ya Msingi.
Mkoa umekuwa na Maendeleo ya kuridhisha ya utoaji taaluma kwa
kutumia kigezo cha matokeo ya mtihani wa kuhitimu Elimu ya
Msingi. Katika kipindi cha 1961 hadi 2010 idadi ya wanafunzi
waliofaulu imeongezeka kutoka 347 hadi 27,899 ikiwa ni ongezeko
la wanafunzi 27,552. Aidha, Mkoa umekuwa ukishika nafasi ya tatu
(3) Kitaifa kwa muda wa miaka 14 mfululizo kuanzia mwaka 1996
hadi 2010.
Jedwali Na. 19: Hali ya kufaulu Mkoani
MWAKA-
WALIOFANYA
WALIOFAULU
(Desemba)
ASILIMIA
(%)
1961/62 616 347 60
1995/96 26,361 18,452 70
2010/11 44,274 27,899 63.01
Chanzo: Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Maendeleo haya ya kitaaluma yamechangiwa na kuongezeka kwa
uwiano kati ya mwalimu na wanafunzi, uwiano wa kitabu na idadi
ya wanafunzi. Vile vile mazingira ya kusomea yameboreshwa kwa
kuongeza vyumba vya madarasa, nyumba za walimu na ujenzi wa
vyoo.
Mpango wa Elimu ya Msingi Kwa Waliokosa (MEMKWA)
Kwa kipindi cha 1961 hadi 2010 Mkoa uliendelea na jitihada za
kuwapatia nafasi ya shule wale waliokosa nafasi hiyo ya kawaida
36
katika shule zetu za msingi chini ya Mpango unaojulikana kama
MEMKWA (Mpango wa Elimu ya Msingi kwa walioikosa).
Hadi
kufikia 2010 kulikuwa na wanafunzi 1,298 katika madarasa/vituo
339
Elimu ya Sekondari
Mwaka 1961 Mkoa ulikuwa na shule za Sekondari zipatazo 6 kati ya
shule hizo, shule 3 ni za Umma (Regional Community and National
Secondary Schools) na 3 ni za Binafsi (Non-Government Secondary
Schools) i.e. Seminari, na za Watu na Mashirika mbalimbali ya
Binafsi. Hadi mwaka, 2010 Mkoa ulikuwa na shule za sekondari 236
kati ya shule hizo, shule 178 ni za Umma (Regional Community and
National Secondary Schools) na 58 ni za Binafsi (Non-Government
Secondary Schools) i.e. Seminari, na za Watu na Mashirika
mbalimbali ya Binafsi.
Ujenzi wa Nyumba ya Mtumishi Kitulo Sekondari-Makete
37
Jedwali Na. 20: Idadi ya Sekondari Kiwilaya (Shule za
Serikali
WILAYA
Umma)
JUMLA SHULE ZILIZOKUWEPO SHULE ZILIZOPO
YA (1961) (2010)
SHULE
KWA
WILAYA
Wananch Serik Madheh Wana Serik Madheheb
i ali ebu ya nchi u ya Dini
ali
Dini
IRINGA - 3
KILOLO - LUDEWA
3
13 40 1
- 4 22 11
- - 2 17 -
MAKETE - - - 14 2
MUFINDI - - 5 41 5
NJOMBE - - 15 41 2
JUMLA - 3 39 175 21
1
4
Chanzo: Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
4.5.2 Afya
Mkoa wa Iringa hadi kufikia mwaka 2010 una jumla ya vituo vya kutolea
huduma za Afya 367 vilivyogawanyika kama ifuatavyo; Hospitali 15,
Vituo vya Afya 41 na Zahanati 311 ikilinganishwa na Mwaka 1961
ambapo Mkoa ulikuwa na Hospitali 3, Zahanati 22 na hakukuwa na Vituo
vya Afya.
Muuguzi akijiandaa kutoa Huduma katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa
38
Ujenzi wa Hospitali ya Manispaa-Iringa
Jedwali Na. 21: Huduma za Afya.
WILAYA
HUDUMA ZILIZOKUWEPO
HUDUMA ZILIZOPO
(1961)
VITANDA
(2010)
Zahanati
Vituo
Hospitali
Zahanati
Hospitali
Vituo
vya vya
Afya
IRINGA
IDADI YA
Afya
22
- 75 11 3 3,789
-
KILOLO
- 3 48 2 1 179
LUDEWA - - - 42 6 3 522
MAKETE - - - 23 4 3 477
MUFINDI - - - 51 8 2 348
NJOMBE - - - 72 10 3 816
22 - 3 311 41 15 6,131
JUMLA
Chanzo: Ofisi ya Mkuu wa Mkoa-Iringa
Lengo la Mkoa katika utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya
Huduma za Afya ya Msingi (MMAM, 2010
2015) ni kuhakikisha
kwamba kila kijiji kuwa na zahanati, kila kata kuwa na kituo cha
Afya na Wilaya kuwa na Hospitali.
Mafanikio mengine yaliyopatikana kuanzia mwaka 1961 hadi 2010
ni:-
·
Ujenzi Nyumba za watumishi wa Afya zimeongezeka kufikia
Nyumba 377 mwaka 2010 kutoka nyumba 10 zilizokuwepo
mwaka 1961.
39
·
Hospitali ya Mkoa nayo ilifanyiwa ukarabati mkubwa na
kujenga Wodi ya kisasa ya Wazazi.
·
Halmashauri za Wilaya ya Iringa na Kilolo zimepata Hospitali
teule za Wilaya.
·
Mahudhurio ya akina mama wajawazito yameongezeka hadi
kufikia asilimia
96 kwa mwaka 2010 ikilinganishwa na
asilimia 5 ya mwaka 1961.
·
Kiwango cha mama wajawazito wanaojifungulia katika vituo
vya tiba imeongezeka kufikia asilimia 88 mwaka 2010
ikilinganishwa na asilimia 5 mwaka 1961.
·
Vifo vitokanavyo na uzazi vimepungua kutoka 578 kwa kila
akina mama 100,000
kufikia
145 kwa kila akina mama
100,000 waliojifungua mwaka 2010.
·
Halmashauri saba (7) kati ya nane (8) zina Bodi za Afya
zenye jukumu la kusimamia ubora wa utoaji wa huduma za
Afya.Halmashauri iliyobaki iko katika hatua za mwisho za
ukamilishaji wa uundaji wa Bodi ya Afya.
·
Idadi ya Vitanda vya kulazia Wagonjwa imeongezeka kufikia
vitanda 6,131.
·
Kiwango cha chanjo kwa watoto wenye umri chini ya mwaka
mmoja kimeongezeka
kufikia asilimia 92 mwaka 2010
ikilinganishwa na asilimia 5 ya mwaka 1961.
·
Vituo vya kutolea wa Dawa za kupunguza makali kwa
wagonjwa wa UKIMWI vimeongezeka kutoka vituo 3 mwaka
2005 kufikia vituo 42 mwaka 2010.
·
Kuboreshwa kwa huduma za Afya za Madaktari bingwa katika
Hospitali ya Mkoa; upasuaji mkubwa, magonjwa ya mifupa,
magonjwa ya akina mama na magonjwa ya watoto.
·
Kuongezeka kwa ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za
Afya kufikia asilimia zaidi ya 80 ya vituo vyote vinavyotoa
huduma.
40
4.5.3 Maji
i. Asilimia ya wakazi wa Mkoa wa Iringa waliokuwa wakipata
huduma ya maji safi na salama Desemba 1961 ni 10%.
Asilimia ya wakazi wanaopata huduma ya maji safi na salama
Desemba 2010 ni 65.4 %.
Ongezeko la asilimia ya wakazi
wanaopata huduma ya maji ni 55.4%.
ii. Idadi ya Kamati za maji zimeongezeka kutoka 0* mwaka 1961
hadi kufikia 434 mwaka 2010.
iii. Mifuko ya maji imeongezeka kutoka Sh. 0* mwaka 1961 hadi
Sh. 90,496,484.50 mwaka 2010.
iv. Idadi ya vituo vya kutekea maji vilivyojengwa au kukarabatiwa
hadi sasa Desemba 2010 ni 7,682.
v. Idadi ya wananchi waliohamasishwa kwa njia ya semina
shirikishi kuhusu usafi wa mazingira ni 161,349
vi. Wahandisi
wa
maji
11
wameajiriwa
na
Halmashauri
na
Sekretarieti ya Mkoa.
vii. Jumuiya ya Watumiaji maji zilizosajiliwa kisheria zimeongezeka
kutoka 0* mwaka 1961 hadi kufikia 21 mwaka 2010.
*Mwaka 1961 Sekta ya Maji haikuwa na Sera inayoelekeza uwepo wa Kamati za
Maji na Mifuko ya Maji.
Mhe.Prof Mark Mwandosya Waziri wa Maji na Umwagiliaji akikagua mradi
wa Maji Mkoani Iringa
41
4.6. Miundombinu na Barabara
4.6.1 Barabara
Mwaka 1961 Mkoa ulikuwa na mtandao wa barabara upatao
Km. 1,209.5 kati ya hizo Km. 76.0 ni barabara za vumbi na
Km. 1,133.5 ni changarawe.
Mtandao huo Desemba 2010
umeongezeka hadi kufikia Km. 8,776.56 kati ya hizo Km. 530.1
ni Lami, Km 5,942.06 ni changarawe na Km.2,304.40 ni
barabara ya udongo.
Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoani Iringa wanahudumia
jumla ya kilometa 2,116 zikiwemo za lami km 510 na za
changarawe km 1,606.
Ukarabati wa barabara za Vijijini ukiendelea Mkoani iringa
4.6.2 Ardhi
Katika kutekeleza Sera ya Ardhi ya mwaka 1995 na Ilani ya
Uchaguzi - Ibara ya 42 Mkoa umeweza kufanya yafuatayo kati ya
1995 na 2010 :-
·
Kukamilisha Upimaji wa mipaka ya vijiji 703 sawa na asilimia
95.5 ya Vijiji vyote 736 vinavyositahili kupimwa.
42
·
Kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa vijiji 97
sawa na asilimia 13.1.
·
Sheria ya Ardhi Na. 5 ya Vijiji imetolewa kwa vijiji 703, vyeti
vya ardhi 442 vimeandaliwa na hati miliki Kimila 3,651
zimeandaliwa.
·
Jumla
ya
viwanja
Makambako,
21,182
Mafinga,
vimepimwa
kitongoji
cha
katika
miji ya
Tungamalenga, Mji
Njombe na Manispaa ya Iringa. Ambapo hati miliki kisheria
zimeandaliwa.
·
Andiko ya mkopo wa Sh. 60,000,000 kwa Halmashauri ya
Manispaa ya Iringa, limewasilishwa Wizara ya Ardhi.
·
Mkoa umeweza kuanzisha mfuko wa kuendeleza upimaji wa
viwanja, na kuweza kuikopesha Manispaa ya Iringa Sh.
29,000,000 Aidha, Wizara ya Ardhi imeweza kuzikopesha
Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Sh. 30,000,000 na Mamlaka
ya mji Mdogo wa Makambako Sh. 40,000,000.Halmashauri ya
Mji Njombe Sh. 55,000,000 na Halmashauri ya Wilaya ya
Iringa Sh. 40,000,000 kwa ajili ya upimaji na uendelezaji wa
Ardhi.
4.6.3. Sekta ya Mipango Miji
·
Imeweza
kuainisha
maeneo
yaliyojengwa
kiholela
katika
Manispaa ya Iringa, Mji Njombe, miji midogo ya Ilula na
Makambako na Mafinga.
·
Kuandaa Mipango ya Kina kwa Maeneo Mapya (Detailed Planning
Schems
for
New
Areas)
kwa
vitongoji
vya
Kidamali,
Tungamalenga, Migoli na Ifunda (Halmashauri ya Wilaya ya
Iringa),
Ilembula, Makambako,
Halmashauri
ya
Wilaya
ya
Njombe, Malangali na Mgololo (Halmashauri ya Wilaya ya
Mufindi).
43
·
Kusimamia uendelezaji wa maeneo ya kati ya Mji (CBD) kwa
maeneo ya Miyomboni, Stendi Kuu na Wilolesi (RETCO) katika
Manispaa ya Iringa.
·
Kutayarisha michoro ya Mipango miji 83 yenye jumla ya Viwanja
33,387 katika miji ya Njombe, Makete, Mafinga, Makambako,
Kidamali, Tungamalenga, Kilolo, Ilula na Manispaa ya Iringa.
4.7. Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
4.7.1. Teknolojia ya Kompyuta
Mwaka 1961 Technolojia ya Kompyuta haikuwepo Mkoani Iringa.
Mwaka 2006 Mkoa na Jumla ya halmashauri tatu za iringa zilianza
kutumia mfumo wa kompyuta (Epicor) kwa ajili ya malipo na
usimamizi wa fedha. Hadi Mwaka 2011 Matumizi ya Mifumo ya
kompyuta ipatayo 8 ilisimikwa kwenye Mkoa na Mamlaka za
Halmashauri zote za Iringa. Mifumo hiyo ni pamoja na Mifumo ya
Mipango na Uratibu (PlanRep, na SBAS), Mifumo ya Mishahara na
Rasilimali watu (Lowson na IHRIS), Mifumo ya Takwimu (MVC
Database, bylaw Database). Hadi kufikia mwaka 2011, Tovuti ya
mkoa (www.iringa.go.tz), Tovuti ya wilaya kilolo (www.kilolo.go.tz),
tovuti ya njombe mji (www.ntc.go.tz) zimeanzishwa na zimeendelea
kufanyiwa maboresho siku hadi siku ili kufanikisha mawasiliano
kimtandao (e- Governement).
Aidha, Hadi kufikia mwaka 2011
asilimia 80 ya watumishi wa umma Mkoani na kwenye halmashauri
wanaweza kutumia kompyuta katika kutekeleza shughuli zao, na
Huduma ya internet imezifikia halmashauri zote za Mkoa wa Iringa
kupitia mtandao wa TTCL, ZAIN, Vodacom, na Zantel.
44
SURA YA 5.
5.0 MAKUNDI MAALUM YALIYOSHUGHULIKIWA KATI YA
1961
2010
5.1 Watoto
Mkoa wa Iringa umekuwa ukifanya jitihada mbalimbali katika
kusimamia haki na ustawi wa mtoto kwa kushirikiana na wadau
mbalimbali na mafanikio yaliyopatikana ni:
i)
Watoto 34,859 wanaoishi katika mazingira magumu
wametambuliwa na wanapatiwa misaada ya kujikimu
ikiwemo mahitaji ya shule (sare na vifaa), mavazi na
matibabu.
ii)
Kamati
618
zimeundwa
ngazi
ya
mtaa/kijiji
ili
kushughulikia matatizo ya watoto walio katika mazingira
hatarishi. Pia mafunzo yametolewa kwa Kamati zote 618
juu ya wajibu wa Kamati na malezi ya watoto.
iii)
Jumla ya Watoto 34,859 wamefaidika na mpango wa
ukomeshaji wa ajira mbaya kwa watoto na kujiunga na
mafunzo ya ufundi, kuwarejesha shuleni na kuhakikisha
wanapata haki zao ikiwa ni pamoja na huduma za Afya,
chakula na mavazi.
5.2 Wazee
i)
Kuna Vikundi vya
wazee vinavyojishughulisha na
shughuli za kiuchumi kama vile kilimo cha mpunga,
mahindi, ufugaji wa nguruwe, ngómbe, mbuzi na kuku
wa kienyeji.
ii)
Wazee wanapata huduma ya matibabu bure katika
hospitali ya Mkoa, Wilaya na katika zahanati na vituo
vya afya vya umma.
iii)
Kuingiza katika Mipango na bajeti shughuli za kusaidia
na kuboresha maisha ya wazee kwa kutenga fedha kila
mwaka ili kuendesha semina za utambuzi wa haki za
45
Wazee kama zilivyoainishwa kwenye Sera ya Taifa ya
Wazee, MKUKUTA na mwongozo wa TASAF.
5.3 Walemavu
i)
Mkoa umetoa
mafunzo
ya
wahudumu
wa
utengamano
(Community Based rehabilitation Workers) 158 katika Halmashauri
zote. Mkoa unasadia jumla ya Walemavu 25 kuanzisha Miradi ya
kilimo,Ufugaji wa kuku,Mbuzi,Nguruwe na Ufugaji wa Nyuki ili
kuwawezesha
kujikwamua
kiuchumi.
Aidha
Mkoa
katika
Halmashauri ya Wilaya ya Njombe ina mkakati wa kuanzisha shule
ya wenye ulemavu wa akili katika Kata ya Makambako.
Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete -Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akitoa
msaada wa Bajaji kwa Bibi Sara Mageni Sanga (Mlemavu aliyeketi) wa Kijiji cha
Lupalilo Wilayani Makete Mkoa wa Iringa tarehe 29 Oktoba, 2009.
46
SURAYA 6.
6.0. HALI YA UKIMWI
Mkoa wa Iringa umeathirika kwa kiwango kikubwa sana na tatizo la
UKIMWI. Kwa mujibu wa matokeo ya utafiti wa hali ya maambukizi
ya VVU na janga la UKIMWI Kitaifa uliofanyika mwaka 2007/2008
maambukizi yameongezeka kutoka asilimia 13.4 mwaka 2003/2004
na kufikia asilimia 15.7.
Aidha, idadi ya Watoto Walio Katika Mazingira Hatarishi pamoja na
wajane inazidi kuongezeka kwa kasi Kubwa, ambapo jumla ya
watoto
68,998
[32,930
Me
na
35,068
Ke]
tayari
wameshatambuliwa, kati ya hao watoto 34,859 sawa na asilimia
52
wanapata misaada mbalimbali
ya
masomo, afya,
malazi
nakadhalika.
6.1 Muelekeo wa mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya VVU
na janga la UKIMWI Mkoani:
Kutokana na ukubwa wa tatizo, Mkoa uliandaa Mpango wa miaka
minne wa utekelezaji wa mapambano dhidi ya ongezeko la
maambukizi mapya ya VVU na janga la UKIMWI [Oktoba, 2008
Septemba, 2012], ambao hadi sasa miaka miwili tayari imeshapita
tangu ulipoanza kutekelezwa.
Aidha, kufuatia uzinduzi wa Mkakati wa Kitaifa wa Kinga 2009
2012 unaolenga kujikita zaidi katika kupunguza maambukizi mapya
ya VVU. Mkoa tayari kupitia ufadhili wa
Restless Development
[SPW] umeshaandaa mpango kazi wa miaka miwili [Julai, 2010
Juni, 2012] na kwa hisani ya Watu wa Marekani ulitambulishwa na
nakala zake kugawiwa kwa wadau wote Mkoani wakati wa kikao cha
wadau kilichofanyika tarehe 29 Novemba, 2010 Mjini Makambako.
47
6.2 Kazi zilizotekelezwa katika kipindi cha mwaka 2009/2010:-
i. Ushauri nasaha na upimaji.
Katika kipindi hicho, jumla ya vituo 132 vilitoa huduma za ushauri
nasaha na kupima. Watu 122,372 walipata ushauri nasaha na
kupima afya zao, kati ya hao 14,745 waligundulika kuwa na
maambukizi ya VVU.
ii. Kuzuia uambukizo wa VVU kutoka kwa mama kwenda kwa
mtoto.
Mkoa una jumla ya vituo 78 vinavyotoa huduma za kupima
maambukizi ya VVU kwa watoto wachanga wanaozaliwa kwa
akinamama wenye maambukizi ya VVU.
Mpaka desemba 2010, Mkoa ulikuwa na jumla ya vituo 333
vya
PMTCT kati ya vituo vya RCH 389 vilivyopo Mkoani. Jumla ya
akinamama
wajawazito
37,210
walipima
afya
zao,
kati
ya
wajawazito 40,855 waliohudhuria hudma hiyo, kati ya hao 5,028
sawa na asilimia 13.5 walipatikana na maambukizi ya VVU. Pia
wenzi wao 16,513 kati ya akinamama 40,855 waliopima afya zao,
wanaume 1,861 sawa na asilimia 11.3 walikuwa na maambukizi ya
VVU.
iii. Udhibiti na usimamizi wa maambukizo ya maradhi ya
ngono
Mkoa una jumla ya vituo 320 vinavyotoa huduma za magonjwa ya
ngono. Katika kipindi hiki, jumla ya watumishi 137 walipata
mafunzo rejea. Sambamba na hilo jumla ya watu 17,268 wenye
magonjwa
ya
ngono
walipatiwa
matibabu.
Magonjwa
haya
yanachangia sana katika maambukizi mapya ya VVU.
iv. Zoezi la Tohara kwa wanaume.
Mkoa wa Iringa ni miongoni mwa Mikoa nane ambayo imeanza
kutoa huduma za tohara kwa wanaume ikiwa ni njia moja wapo ya
kupunguza maambukizi ya VVU kwa wanaume. Mkoa wa Iringa
ulianza kutoa huduma hizi septemba 2009, kwa kushirikiana na
48
Shirika la JHPIEGO na Wizara ya Afya. Mpango huu umeanza
kutekelezwa katika Halmashauri za Iringa, Mufindi na Iringa
Manispaa. Mpaka Disemba 2010 wanaume 17,433 wametahiriwa.
Hii ni sehemu ndogo sana ya watu wanaotakiwa kutahiriwa ili
kupunguza maambukizi ya VVU katika jamii. Mkoa unatakiwa
kutahiri jumla ya wanaume 264,990 katika kipindi cha miaka 5 .
v. Kutoa Tiba kwa wagonjwa wa UKIMWI na watu wanaoishi
na VVU
Tiba kwa waishio na VVU/UKIMWI hutolewa katika Halmashauri zote
Mkoani. Mkoa mpaka sasa una jumla ya vituo 81 ambavyo
vimepewa kibali cha kutoa huduma hizo. Kati ya vituo hivyo 42
vinatoa huduma.
Vituo
39 vimeanzishwa mwaka 2010
na
vimepasishwa na Wizara afya na ustawi wa jamii kutoa huduma
hizo.
Halmashauri
zimekuwa
taratibu
sana
katika
kuanzisha
huduma hizo katika vituo hivyo vipya. Mpaka Disemba jumla ya
waishio na VVU/UKIMWI 74,632 wameandikishwa, kati ya hao
40,287 sawa na asilimia 54 wameanza kutumia dawa.
vi. Kutoa huduma za Mseto wa wagonjwa wa Kifua Kikuu na
VVU
Mpaka Disemba 2010, Mkoa ulikuwa na jumla ya vituo 63
vinavyotoa huduma mseto. Katika kipindi hiki, vituo viliripoti jumla
ya wagonjwa wa Kifua Kikuu 3,168. Kati ya hao 2,902 sawa na
asilimi 91.6 walikubali kupima VVU. Kati ya hao 1,735 sawa na
asilimia 59.8 walikuwa na maambukizi ya magonjwa yote mawili.
Wagonjwa hao walipata tiba sahihi katika vituo husika.
vii.
Utoaji
wa huduma majumbani
kwa wagonjwa wa
UKIMWI [magonjwa ya kusendeka] na wengine wanaoishi na
VVU.
49
Huduma
hii
ilitekelezwa
Mkoani
mbalimbali kama vile FHI
kwa
kushirikiana
na
wadau
Tunajali, AMREF na wengineo. Pia
Mpango wa Taifa umetoa mfumo mpya wa ukusanyaji taarifa za
magonjwa majumbani ambao utaziwezesha Halmashauri kupata
idadi kamili ya watu waliopata huduma hizo.
viii. Mikutano ya uhamasishaji jamii juu ya mapambano
dhidi ya VVU/UKIMWI
Katika kipindi hiki jumla ya mikutano 287 ya uhamasishaji katika
ngazi ya Jamii ilifanyika, vikundi 193 vya Kijamii vilishiriki na jumla
ya
Vipeperushi
na
Mabango
19,500
ya
kuelimisha
Jamii
vilisambazwa kwa wananchi,
ix. Elimu juu ya matumizi sahihi ya Kondom
Elimu ilitolewa na jumla ya Paketi 13,435 za Kondomu zilitolewa na
Watu 217,514
walifikiwa na elimu ya matumizi sahihi ya
Kondomu,
xi. Mikutano ya uhamasishaji jamii juu ya Mila na desturi
potofu
Katika kipindi cha 2009/2010 jumla ya mikutano 176 ya kujadili
Mila na Desturi hatarishi ilifanyika katika ngazi ya Jamii,
xii.
Kujengea uwezo Kamati za UKIMWI
Jumla ya Kamati 48 za Kudhibiti UKIMWI ngazi ya Wilaya
zilijengewa uwezo, zikijumuishwa CMAC 8 na WMAC 40
xiii. Uratibu wa shughuli za UKIMWI ngazi zote
Jumla ya Viongozi 1,451 katika Kada na ngazi mbalimbali Mkoani
walijengewa uwezo na ziara 2 za mafunzo juu ya utekelezaji wa
50
shughuli za mapambano dhidi ya UKIMWI zilifanyika nje ya Mkoa
wa Iringa,
xiv. Kuhamasisha na kuelimisha jamii kupitia gari maalum
la Sinema
Katika kipindi hiki cha taarifa, jumla ya Vijiji 109 kati ya 737
vilifikiwa, Mitaa 162 kati ya 206 ilifikiwa sambamba na Shule za
Msingi 13 kati ya 922 zilifikiwa. Jamii kwa ujumla imehamasika na
kuvutiwa sana na elimu inayotolewa kupitia gari hilo,
xv.
Kampeni za mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
Zimefanyika Kampeni mbalimbali za kupambana na ongezeko la
maambukizi ya VVU na UKIMWI, Kampeni hizo ni;
 ̈ Kampeni ya Kondomu aina ya Dume na Salama,
 ̈ Kampeni ya Tohara kwa wanaume,
 ̈ Kampeni ya Ishi,
 ̈ Kampeni ya
Champion
Wanaume kuwajibika katika masuala
ya afya na uzazi wa Mpango,
 ̈ Kampeni ya upimaji wa VVU kwa hiari,
 ̈ Kampeni ya kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama
kwenda kwa mtoto n.k.
6.3 Mafanikio yaliyopatikana:
a) Kujenga mahusiano mazuri na Wabia/Wadau wa mapambano
dhidi ya janga la UKIMWI Mkoani,
b) Mwamko wa jamii katika masuala ya kujitokeza kupatiwa ushauri
nasaha na kupima VVU kwa hiari,
c) Kuongeza idadi ya vituo vya CTC katika kila Halmashauri,
51
d) Mwitikio mkubwa katika Kampeni za tohara kwa wanaume,
e) Kupanua huduma za PMTCT kufikia zaidi ya asilimia 86,
6.4 Changamoto:
a) Ongezeko kubwa la kiwango cha maambukizi ya VVU Mkoa wa
Iringa bado ni kitendawili. Huenda kuna sababu za msingi
ambazo bado hazijafanyiwa uchambuzi wa kina na kufanyiwa
kazi,
b) Mila na desturi hatarishi bado inaonekana kuwa ni tatizo katika
Mkoa,
c) Baadhi ya wanajamii kutokuwa tayari kubadili tabia na kuishi
maisha salama,
d) Ongezeko
kubwa
la
yatima,
wajane
na
waathirika
wa
VVU/UKIMWI,
e) Uhaba wa rasilimali fedha katika kutekeleza afua za UKIMWI,
f) Baadhi ya Wadau/Wabia kutokuwa tayari kutoa taarifa za
matumizi ya fedha wanazopewa na Wafadhili kwa ajili ya
mapambano.
g) Kukosekana kwa mwamko wa kutambua majukumu na wajibu
wetu wa kuwatunza na kuwasaidia Watoto walio katika mazingira
hatarishi [WWKMH] na badala yake kutegemea zaidi misaada
kutoka kwa wafadhili,
h) Mwamko mdogo wa akina baba kushiriki kwenye huduma za
PMTCT,
i) Kukosekana kwa uwazi juu ya fedha zinazotolewa kwa wadau
kwa ajili ya matumizi ya mapambano dhidi ya UKIMWI,
j) Sekreatrieti ya Mkoa na Halmashauri zimekuwa zikipata fedha
kidogo
kuliko
bajeti
iliyopangwa
zinazopangwa kushindwa kutekelezwa,
52
hivyo
shughuli
nyingi
k) Halmashauri
kutoanzisha
huduma
za
CTC
katika
vituo
vilivyochaguliwa na kupewa namba za CTC.
l) Upungufu wa Vitendanishi wa upimaji wa VVU/UKIMWI,
m) Vijiji vingi havijafikiwa na elimu kwa njia ya sinema kwa sababu
ya ufinyu wa rasilimali fedha,
6.5 Matarajio
Serikali ya Mkoa itaendelea kuelekeza nguvu zaidi za mapambano
katika Mpango wake wa utekelezaji
na Mapango Kazi kwa
kuzingatia Mkakati mpya wa Kitaifa wa Kinga, ambapo mambo
yafuatayo yatapewa kipaumbele:
i. Kuongeza elimu na uhamasishaji juu ya masuala ya ngono
salama kwa makundi yaliyo katika mazingira hatarishi,
ii. Kuhakikisha upatikanaji wa kutosha na kuendelea kutoa elimu
juu ya matumizi sahihi ya Kondom,
iii. Kuendesha Kampeni na elimu juu ya umuhimu wa tohara
[kutahiri] kwa wanaume,
iv. Kuzijengea jamii uwezo wa kupambana na Mila na desturi
hatarishi zinazochangia ongezeko la maambuki mapya ya VVU,
v. Kupeleka karibu na kuboresha huduma za afya kwa jamii,
vi. Kuboresha huduma za magonjwa ya zinaa,
vii.
Kuwajengea uwezo Wataalam wa afya wa kujikinga na
kuchukua tahadhari ya maambukizo wanapokuwa kazini,
viii.
Kuimarisha na kuboresha upatikanaji na utoaji wa taarifa za
mapambano dhidi ya UKIMWI,
ix. Kujengea uwezo Kamati za UKIMWI katika ngazi zote,
x. Kuimarisha Uratibu wa shughuli za UKIMWI ngazi zote,
xi. Kuendelea kujenga na kuimarisha mahusiano mazuri yaliyopo
sasa na Wadau, ASASI za Kiraia na Wabia mbalimbali wa ndani
na nje ya Mkoa.
53
54
SURA YA 7.
7.0 MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA
Mwaka 2009/10 jumla ya taarifa 861 za rushwa zilipokelewa
na kufanyiwa kazi katika hatua mbalimbali za kiuchunguzi na
kiutawala. Jumla ya taarifa 188 zilifunguliwa majalada na
taarifa 85 zilifungwa baada ya uchunguzi kubaini kutokuwepo
kwa makosa ya rushwa. Kwa upande wa elimu kwa umma
mwaka
2010
TAKUKURU iliweza
kutoa
elimu
kwa
njia
mbalimbali ikiwemo kufanya mijadala ya wazi 7, maonesho,
semina na utoaji wa machapisho 23,235 ya TAKUKURU yenye
ujumbe
mbalimbali
kuhusu
rushwa.
Pia,
TAKUKURU
imefanikwa kufungua vilabu vya wapinga rushwa katika shule
za sekondari 120 kati ya 216 na shule nyingine zipo katika
hatua mbalimbali za ufunguzi.
Jumla ya wanachama 54,398 wamejiunga katika vilabu vya
wapinga rushwa.
55
SURA YA 8.
8.0 CHANGAMOTO MBALIMBALI:
Kwa
kipindi
cha
1961
hadi
2010
changamoto
kuu
zilizojitokeza ni pamoja na:
(i)Kuchelewa kupata fedha za matumizi ya kawaida na miradi
ya Maendeleo,
(ii)Kutokuwepo na mipango madhubuti ya mafunzo ya
Technohama kwa wataalam wa ICT na watumiaji wa mifumo
ya Teknohama.
(iii) kutokuwepo na vifaa na miundombinu ya kutosha ya
Technohama kwenye RS na Halmashauri
(ii)Kupanda kwa bei za pembejeo za kilimo,
(iv)Kutopatikana dawa muhimu katika kitengo cha MSD
wakati wote,
(v)Upungufu wa miundombinu katika shule za msingi na
sekondari na
(vi)Maambukizi ya UKIMWI yameendelea kuwa changamoto
kubwa.
Hatua zilizochukuliwa kukabiliana na changamoto hizi ni kama
ifuatavyo:
(i) Kuwasiliana na Wizara ya Fedha ili fedha ziletwe mapema,
(ii)Kuweka mpangilio mzuri na matumizi kwa fedha kidogo
iliyopatikana,
(iii) Kuwapatia Wataalamu mafunzo mbalimbali, na
(iv) Mipango shirikishi iliandaliwa kwa kuzingatia vipaumbele.
56
SURA YA 9.
9.0: MATARAJIO YA MKOA KATIKA MIAKA 50 IJAYO:
Katika Miaka 50 ya Uhuru Mkoa umeweza kupata mafanikio
makubwa
katika
kutekeleza
majukumu
yaliyopangwa
katika Mipango iliyomo katika Ilani ya CCM na maagizo ya
Serikali. Mafanikio haya yanatokana na michango ya
Wananchi, Viongozi, Watendaji na Wadau mbalimbali wa
Sekta ya Umma na Sekta binafsi. Tunatarajia katika Miaka
50 ijayo tutapiga hatua kubwa zaidi.
57

Thursday, August 2, 2012

HOTUBA YA MHE. DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE,

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,

KWA WANANCHI, TAREHE 31 JULAI, 2012

Ndugu Wananchi;

Naomba nianze kwa kuomba radhi kwa kutoa hotuba ya mwisho wa mwezi wa saba, leo tarehe 01 Agosti, 2012 badala ya jana tarehe 31 Julai, 2012. Hii ni kwa sababu ya msiba uliotukuta katika familia na mimi kwenda Lindi kushiriki maziko ya marehemu wetu. Tofauti na miezi iliyopita leo, pamoja na hotuba ya kawaida ya mwisho wa mwezi nimetoa fursa kwa Wahariri wa vyombo vya habari nchini kuniuliza maswali nami kujibu. Kwa upande wangu nina mambo matatu ambayo nitayazungumzia leo.

Ajali ya Kuzama kwa Meli ya MV SKAGIT

Ndugu Wananchi;

Jambo la kwanza ni ajali ya Meli ya MV SKAGIT iliyotokea tarehe 18 Julai, 2012. Meli hiyo ilikuwa na watu 290, wakiwemo mabaharia 9, abiria watu wazima 250 na watoto 31. Juhudi za uokoaji zilianza mara baada ya taarifa ya kuzama kwa meli hiyo kupatikana. Maofisa na askari wa JWTZ, Polisi na KMKM walishiriki pamoja na meli na watu binafsi katika uokoaji. Waokoaji walifanikiwa kuwapata ndugu zetu 146 wakiwa hai na maiti 126 hadi tarehe 27 Julai, 2012. Kwa maana hiyo basi, watu 18 hawajulikani walipo na inahofiwa kuwa nao pia hawako hai. Huenda wamezama pamoja na meli au walizama baharini lakini miili yao haikuweza kupatikana.

Ndugu Wananchi;

Napenda kutumia nafasi hii kurudia kutoa mkono wa rambirambi na pole nyingi kwa wale wote waliopoteza ndugu, jamaa na marafiki katika ajali ile. Nampongeza sana Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein na viongozi wenzake wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kwa kazi kubwa na nzuri waliofanya kuongoza juhudi za uokoaji pamoja na huduma walizotoa kwa waliokolewa, waliojeruhiwa na waliofariki. Kwa wale ambao walikuwa wenyeji wa Unguja na Pemba, SMZ ilitoa sanda na usafirishaji wa maiti mpaka makwao kwa mazishi. Kwa wale wasiokuwa na ndugu Serikali ilibeba jukumu la kuwazika kule Kama, Kusini Unguja.

Natoa pongezi za pekee kwa wale wote walioshiriki katika uokoaji kwani juhudi zao ziliwezesha ndugu zetu wengi kusalimika na maiti nyingi kupatikana.

Ndugu Wananchi;

Kutokea kwa ajali ile kumetonesha jeraha la huzuni, majonzi na mashaka makubwa yaliyolipata taifa letu miezi 11 iliyopita kufuatia ajali ya kuzama kwa meli ya MV Spice Islander. Katika mkutano maalum wa Baraza la Usalama wa Taifa niliouitisha tarehe 20 Julai, 2012 kuzungumzia ajali ya MV SKAGIT tulifanya mapitio ya utekelezaji wa maagizo yetu ya mkutano wa tarehe 11 Septemba, 2011 kufuatia ajali ya MV Spice Islander. Kwa ujumla tumeridhika kuwa utekelezaji umekuwa mzuri kwa upande wa mamlaka zinazohusika na usafirishaji majini yaani SUMATRA, Zanzibar Maritime Authority na mamlaka za Bandari za nchi zetu mbili. Ushirikiano baina ya mamlaka hizo sasa ni mzuri kwa mambo yote muhimu ambayo Baraza liliagiza wafanye hivyo. Pamoja na hayo Baraza limetaka ushirikiano huo uzidishwe na kuimarishwa.

Kwa mfano, Baraza limefurahishwa na kupongeza kitendo cha mamlaka hizo kutumia Dar es Salaam Maritime Institute kwa ushauri kuhusu ubora wa meli na huduma za usafirishaji majini. Baraza limeagiza vyombo hivyo viwe na hadidu za rejea zinazofanana kwa vigezo vya ubora ili nchi yetu iwe na viwango vinavyofanana vya ubora wa meli na huduma za usafirishaji baharini kwa pande zetu mbili za Muungano. Bahari ni moja na vyombo vinahudumia watu wale wale, kuwa na vigezo tofauti vya ubora wa meli na viwango vya huduma ni jambo lisilostahili kuwepo tena, ni la hatari. Baraza pia limeagiza pawepo na ukomo wa umri wa meli zilizokwishatumika zinazoruhusiwa kutumika hapa nchini.

Aidha, Baraza limerudia kuagiza pawepo na usimamizi makini zaidi kuhusu upakiaji wa mizigo na abiria. Mamlaka husika, yaani SUMATRA, ZMA na maofisa wa bandari wahakikishe kuwa uwezo wa meli uliohakikiwa na kutambuliwa unaheshimiwa ipasavyo. Pia, meli zikaguliwe mara kwa mara na vigezo vifanane.

Ndugu Wananchi;

Pamoja na hayo, Baraza la Usalama wa Taifa limeona kuwa wakati umefika kwa Serikali yetu kuwa na Coast Guards, yaani kikosi maalum cha uokoaji na usalama majini. Aidha, Baraza limetaka hatua za makusudi zichukuliwe kuimarisha KMKM na Police Marines. Mwisho, Baraza lilipongeza uamuzi wa SMZ wa kuunda Tume ya kuchunguza ajali ile kama ilivyofanya wakati wa ajali ya MV Spice Islander.

Utafutaji na Uchimbaji Gesi Nchini

Ndugu Wananchi,

Jambo la pili ninalopenda kulizungumzia leo ni kuhusu maendeleo ya sekta ya gesi asili nchini. Juhudi za kutafuta mafuta nchini zilianza mwaka 1952 na mwaka 1954 wakati kampuni ya BP ilichimba kisima cha kwanza kule Mafia. Bahati mbaya kisima hicho hakikuzaa matunda yaliyotarajiwa na juhudi za utafutaji mafuta zikafifia kabisa mwanzoni mwa miaka ya 1960. Miaka kumi baadae, juhudi hizo zilianza upya na kuendelea kwa kiwango na kasi za namna mbalimbali hadi sasa. Katika miaka ya hivi karibuni juhudi zimekuwa kubwa na kuhusisha makampuni kadhaa ya kimataifa yakiwemo makubwa na madogo.

Ndugu Wananchi;

Tangu mwaka 1954, mpaka sasa visima 61 vimechimbwa, kati ya hivyo, gesi asili imegunduliwa katika visima 22, visima 14 vya nchi kavu na maeneo ya maji mafupi na visima 8 vya bahari ya kina kirefu. Hatujabahatika kupata mafuta lakini tumefanikiwa kupata gesi asili katika maeneo kadhaa baharini na nchi kavu katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Pwani.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo kutokana na visima vilivyochimbwa mpaka sasa, akiba ya gesi asili iliyopo nchini inakadiriwa kuwa kati ya futi za ujazo trilioni 25.4 – 28.9. Yapo matumaini makubwa ya gesi nyingi zaidi kugundulika katika miaka michache ijayo. Hii ni kutokana na ukweli kwamba shughuli za utafutaji mafuta na hasa gesi baharini zilizoanza mwaka 2004 kukiwa na kampuni moja sasa zipo 18. Baada ya ugunduzi wa kwanza wa gesi mwaka 2010, shughuli za utafutaji sasa zimepamba moto na zimekuwa na mafanikio. Naamini gesi nyingi zaidi itaendelea kupatikana.

Fursa za Maendeleo

Ndugu Wananchi;

Kwa kiasi cha gesi asili kilichokwishagunduliwa na kwa matumaini yaliyopo ya gesi zaidi kupatikana kunaifanya Tanzania kuwa moja ya nchi za kutumainiwa duniani kwa upatikanaji wa gesi asili miaka michache ijayo. Hali hiyo inaipa nchi yetu fursa kubwa ya kuweza kujiletea maendeleo makubwa ya kiuchumi na kijamii muda si mrefu kutoka sasa.

Gesi asili ni rasilimali inayoweza kutumika kuzalisha mbolea na hivyo kusaidia katika kuendeleza kilimo nchini kwa kurahisisha upatikanaji wake na kuwa ya bei nafuu. Gesi asili inaweza kutumika kuzalisha umeme na hivyo kuiwezesha nchi kupata umeme wa kutosha na kuwepo ziada ya kuuza nje. Hivi sasa, katika gridi ya taifa megawati 350 za umeme zinatokana na gesi asili na hata lengo letu la kuzalisha megawati 3,500 ifikapo maka 2015 tunategemea zaidi gesi asili kuwezesha hilo kutimia. Ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara kuja Dar es Salaam una shabaha hiyo.

Ndugu Wananchi;

Vile vile, gesi asili inaweza kutumika kutoa nishati viwandani badala ya kutumia mafuta na hivyo kupunguza gharama za uzalishaji. Watu majumbani wanaweza kutumia gesi asili kupikia hivyo kupunguza matumizi ya umeme, mafuta, mkaa na kuni. Inapunguza gharama za maisha na kusaidia kuhifadhi mazingira kwa kupunguza ukataji wa miti. Ni kutokana na kutambua ukweli huo ndiyo maana TPDC inatekeleza mradi wa kutengeneza gridi ya mabomba ya kusambaza gesi majumbani katika jiji la Dar es Salaam.

Jambo lingine muhimu kuhusu rasilimali hii ni kwamba tukiuza nje gesi nchi yetu itapata mapato mengi tena ya fedha za kigeni. Kwa vile gesi ni nyingi mapato ya Serikali yataongezeka sana, hivyo kuijengea uwezo wa kutimiza majukumu yake vizuri zaidi. Kama matumizi yatakuwa mazuri, gesi asili itakuwa kichocheo kikubwa cha kukuza uchumi wa nchi. Maendeleo ya haraka yatapatikana na hivyo kusaidia kuwaondoa wananchi wengi kutoka katika lindi la umaskini tulionao sasa.

Changamoto Muhimu

Ndugu Wananchi;

Pamoja na ukweli kwamba kuwa na gesi asili nyingi kunaipa nchi yetu fursa kubwa ya kujiletea maendeleo, zipo pia changamoto zake. Hatuna budi kuzitambua na kuzitafutia ufumbuzi ili gesi iweze kunufaisha ipasavyo nchi yetu na watu wake. Changamoto zipo nyingi lakini kubwa zipo za namna tatu.

Changamoto ya kwanza ni ile ya kujenga uwezo wetu wenyewe wa kudhibiti shughuli zinazofanywa na makampuni ya mafuta ili tuhakikishe kuwa tunapata malipo yanayostahili. Inatulazimu tuwe na wataalamu wetu wazalendo wa fani za taaluma zihusuzo gesi kama vile uhandisi, kemia, jiofizikia, uhasibu, ukaguzi na sheria. Tusipojenga uwezo wetu wenyewe kwenye maeneo hayo kuna hatari ya kudhulumiwa na kupata hasara. Pengine ipo haja ya kuwa na chombo maalum kwa ajili hiyo kama tulivyofanya kwa mafanikio kwa upande wa dhahabu.

Changamoto ya pili ni ile ya kupata Watanzania wengi wenye ujuzi na taaluma zinazohitajika na soko la ajira la sekta ya gesi. Tusipofanya hivyo makampuni yataajiri watu hao kutoka nje na hivyo kufanya Watanzania kutokunufaika na fursa za ajira zilizopo.

Ndugu Wananchi,

Kwa changamoto hizi mbili, jawabu lipo kwenye elimu na mafunzo tunayotoa kwa vijana wetu katika shule, vyuo vya ufundi na vyuo vya elimu ya juu. Kwanza kabisa lazima tuboreshe elimu ya sayansi na hisabati katika shule zetu za msingi na sekondari. Katika vyuo vya ufundi tutoe mafundi mchundo wa taaluma zinazohitajika na tasnia ya gesi na mafuta. Hivyo hivyo kwa upande wa vyuo vikuu nako wafundishe wataalamu wa fani zinazohitajika kama vile utafutaji wa gesi na mafuta, uendelezaji wa mafuta na gesi, uchumi na biashara ya mafuta na gesi, uhasibu na ukaguzi wa mafuta na gesi pamoja na sheria za mafuta na gesi na mikataba ya utafutaji na uendelezaji wa mafuta na gesi.

Ndugu Wananchi;

Napenda kuwahakikishia kuwa tayari tumejipanga kutafuta ufumbuzi wa changamoto hizo. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinajiandaa kuanza kutoa mafunzo ya Chemical and Environmental Lab for Oil and Gas na fani ya Exploration and Production Software Technology katika mwaka huu wa masomo. Chuo cha Madini Dodoma kitaanza kutoa mafunzo ya diploma ya Petroleum Geoscience kuanzia Septemba mwaka huu. Chuo Kikuu cha Dodoma, Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Arusha, na Chuo cha Teknolojia cha Mbeya na kile cha Dar es Salaam pia wameanza kufundisha mitaala hiyo. Aidha, VETA Makao Makuu na VETA Mtwara nao wanafundisha masomo yahusuyo gesi. Wizara ya Nishati na Madini itawadhamini wanafunzi 50 kutoka Mkoa wa Mtwara kwenda kupata mafunzo hayo ya gesi asili katika chuo cha VETA Mtwara.

Ndugu Wananchi;

Wizara ya Nishati na Madini pia inatekeleza mpango mkakati wa kuwapata wataalamu wa sekta hiyo kati ya 40-50 kati ya sasa na mwaka 2016. Taaluma zinazotiliwa mkazo ni Petroleum Geoscience, Petroleum Geophysics, Petroleum Geochemistry, Petroleum Engineering, Petroleum Modeling, Oil and Gas economics, Oil and Gas Accounting and Auditing na Oil and gas Legal Regimes and Contract Negotiations. Kwa upande wake, Serikali itatoa upendeleo maalum kwa kulipia gharama zote za mafunzo ili tuweze kuwapata wataalamu hawa mapema iwezekanavyo. Nawaomba vijana wetu wachangamkie fursa hizi za masomo na watakapohitimu mafunzo wawe tayari kuitumikia nchi yetu kwa bidii.

Kujenga Uwezo Wetu wa Kutumia Mapato ya Gesi

Ndugu Wananchi,

Changamoto nyingine kubwa sana ni ile ya kuhakikisha kuwa mapato yatokanayo na gesi yanatumika vizuri na kwa manufaa ya taifa na watu wake. Lazima tuanze sasa kufikiria na kujipanga kwa ajili hiyo. Si vyema tukangojea mpaka hapo mapato yatakapoanza kupatikana ndiyo tufikirie na kutengeneza mfumo mzuri wa kusimamia na kutumia mapato yatokanayo na gesi. Tutakuwa tumechelewa, watu laghai na waovu watakuwa wameanza kunufaika hivyo watakuwa wagumu kutengeneza mfumo utakaowanyima fursa ya kuliibia taifa.

Jambo hili ni muhimu sana kufanya kwani ipo mifano hai ya nchi zenye rasilimali nyingi za mafuta na gesi lakini nchi na wananchi wake hawanufaiki sawia. Mauzo yanafanyika na fedha nyingi kupatikana lakini manufaa kwa nchi na watu wake ni madogo au hayapo kabisa. Wanaonufaika ni viongozi na baadhi ya maofisa wa umma wanaohusika na usimamizi wa shughuli zihusuzo rasilimali hizo. Na, hata sisi tunaweza kujikuta katika hali hiyo kama tusipojipanga vizuri sasa ambayo badala ya rasilimali kuwa baraka zinageuka kuwa balaa au hata laana.

Ndugu Wananchi;

Zipo nchi duniani ambazo zina usimamizi mzuri wa mapato ya rasilimali za mafuta na gesi na kuleta baraka na neema kwa taifa na watu wake. Nchi hizo zimeweza kuhifadhi na kutumia vizuri mapato yake kukuza uchumi wa nchi kwa jumla na kuboresha upatikanaji wa huduma za kiuchumi na kijamii kwa watu. Matokeo yake ni watu wa nchi hizo kuishi maisha yaliyo bora kuliko walivyokuwa kabla ya kupatikana kwa rasilimali hizo. Lakini, hii imewezekana kutokana na usimamizi mzuri na matumizi mazuri ya mapato yatokanayo na mafuta na gesi.

Tumeamua kujifunza kutoka nchi za wenzetu waliofanikiwa ili na sisi tunufaike. Na sisi tunajiandaa kutengemeza Sera ya Gesi Asili na kurekebisha Sheria ya Utafutaji na Uzalishaji wa Mafuta na Sheria ya Menejimenti ya Mapato ya Serikali yatokanayo na gesi zitakazotoa majibu hayo na kuliwezesha taifa kuwa na mfumo mzuri wa usimamizi wa utafutaji na uchimbaji wa gesi asili pamoja na usimamizi na matumizi mazuri ya mapato yatokanayo na gesi hiyo. Wapo wenzetu kwa mfano, wanacho kitu kinachoitwa Sovereign Funds ambapo mapato yote huhifadhiwa na baadae hutolewa kwa utaratibu maalum. Tunataka tujifunze kutoka kwao ili na sisi tutengeneze chombo chetu cha namna hiyo ili tunufaike.

Ndugu Wananchi;

Mambo hayo tumeshaanza kuyafanyia kazi. Katika mazungumzo yangu na baadhi ya wakuu wa nchi rafiki na mashirika ya maendeleo ya kimataifa, nimewasilisha maombi ya kusaidiwa na kushirikiana kwa mambo mawili. Kwanza kwa kuwawezesha Watanzania kupata mafunzo ya haraka kwa wataalamu watakaosaidia kusimamia shughuli za utafutaji, uendelezaji na biashara ya gesi asili nchini. Pili, watusaidie kupata watu wenye ujuzi na uzoefu ili watushauri kuhusu namna ya kutengeneza mifumo bora ya kusimamia na kutumia mapato ya gesi kwa mujibu wa mifano ya wenzetu waliofanikiwa. Nafurahi kwamba maombi yetu yamepokelewa vizuri na nchi zote na mashirika yote ya kimataifa tuliozungumza nao. Baada ya muda si mrefu kazi itaanza.

Mgomo wa Walimu

Ndugu Wananchi;

Jambo la tatu na la mwisho ni mgomo wa walimu. Pengine ni mapema kusema kwa vile kesho Mahakama itaamua kuhusu shauri hilo. Lakini napenda kuwahakikishia walimu kuwa tunawajali, tunawathamini na kutambua mchango wao muhimu kwa taifa letu. Wakati wote tumekuwa tunashughulikia madai ya haki zao na malimbikizo mbalimbali. Madai ya safari hii ni makubwa mno, yametuzidi kimo. Athari za kuyatimiza yalivyo yataifanya bajeti ya Serikali kutumia asilimia 75 kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa Serikali na kubakiza asilimia 25 kwa kuendeshea Serikali na kutimiza majukumu ya maendeleo kwa wananchi. Haitakuwa sawa. Ndiyo maana tumeshindwa kuelewana walipokataa rai hiyo na wao kusisitiza kugoma.

Wakati tunaendelea kusubiri uamuzi wa Mahakama, nina maombi mawili kwa walimu: Moja, wasiwalazimishe walimu wasiotaka kugoma wafanye hivyo, wawaache waendelee na kazi. Pili, wasitumie watoto isivyostahili kujenga hoja zao. Nawasihi warudi kwenye meza ya mazungumzo.

Ndugu Wananchi;

Kabla ya kumaliza hotuba yangu naomba nitumie fursa hii kuwatakia Waislamu wote nchini kheri na baraka tele kwa swaumu ya mwezi mtukufu wa Ramadhan. Wakati wote, mjiombee wenyewe kwa Mwenyezi Mungu awajaalie toba na malipo mema katika mfungo huu. Mkumbuke pia kuiombea nchi yetu amani, upendo na mafanikio mema.

Baada ya maneno hayo, naomba sasa niishie hapo. Nawashukuru sana kwa kunisikiliza. Sasa nipo tayari kujibu maswali ya Wahariri kama yapo. Ndugu Wahariri mliopo hapa, karibuni.